THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

INTRODUCING: SSK GROUP - Habari Ya Leo

SSK ni kundi jipya la Hip Hop linaloundwa na Wakazi, Zaiid, P The MC na Cjamoker (Producer). Muunganiko wa emcees hawa wenye ladha tofauti nao umeweza kuzaa kitu tofauti ambacho hakijazoeleka kutoka kwao wakiwa wanafanya kazi as solo artists.

Wakizoeleka kama punchline rappers, SSK kwa ujumla wamefanikiwa kubadilisha dhana hiyo na kuweza kufanya Muziki ambao unalenga mambo ya kijamii hususan Mahusiano, Uchumi, Furaha, Imani na Mapito ya maisha na kadhalika, na wamefanikiwa kufanya hivyo kwa kutumia lugha nyepesi na bado kwa kuzingatia misingi ya Muziki wa Hip Hop. SSK inatarajia kuwaonesha mashabiki upande wa pili wa rappers hawa ila pia kuwa funzo la umoja, hususan katika kipindi hiki ambacho makundi na umoja wa Wasanii unavunjika kila siku.

Jina la SISI SIO KUNDI lilikuja kiutani ila lina maana kwa sababu, kila msanii ataendelea kuwa na individual brand ila umoja unakuja pale wanapofanya kazi kama SSK. Ila pia sisi sio kundi sababu ni zaidi ya kundi, maana malengo yetu tunayotarajia kuyafikia ni kuwa zaidi ya kundi la muziki.

Kundi lilizaliwa wakati wa utayarishaji wa wimbo wa "Cjamoker" ambao marapper wote hawa walishiriki. Wimbo rasmi wa utambulisho wa kundi unaitwa "Habari Ya Leo" na tayari SSK wapo kwenye hatua za mwisho Za uandaaji wa Album yao itakayoitwa "SISI SIO KUNDI". Mabibi na Mabwana nawaletea kwenu... SSK!!