Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Umoja wa Afrika katika Usuluhishi wa Mgogoro wa Libya, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amefanya ziara Mashariki mwa Libya tarehe Mei, 11 2017.

Katika ziara hiyo, Rais Mstaafu Kikwete amekutana na Spika wa Baraza la Wawakilishi (House of Representative), Agila Saleh Essa Gwaider  nyumbani kwake Al-Qubba, Libya.

Katika mazungumzo yao, Rais Mstaafu amemuhakikishia utayari wa Umoja wa Afrika kushirikiana na pande zote za Libya kuwezesha kufikiwa kwa suluhu ya kudumu. Amempongeza kwa dhamira na utayari wake wa kutafuta suluhu kwa njia ya mazungumzo katika muktadha wa Mkataba wa Amani wa Libya (Libya Political Agreement).

Kwa upande wake, Spika Aguila amemshukuru Rais Mstaafu Kikwete kwa kufanya ziara kwa mara ya kwanza Mashariki mwa Libya tokea kutokea kwa mapinduzi nchini humo. Ameelezea imani yake kubwa kwa Umoja wa Afrika na mchango wake katika kutafuta suluhu ya kudumu ya tofauti zilizopo miongoni mwa wadau wa siasa wa Mashariki na Magharibi mwa Libya. Amemuhakikishia Rais Mstaafu utayari wake na wenzake wa kupitia upya baadhi ya vipengele vya Mkataba kwa lengo la kuuimarisha na si kuandikwa kwa Mkataba mpya.
Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Umoja wa Afrika katika Usuluhishi wa Mgogoro wa Libya, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi Libya (House of Representative),Agila Saleh Essa Gwaider baada ya mazungumzo yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...