Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania,
Mhe. Prof. Ibrahim Juma akisamiliana na Watumishi wa Mahakama, Kanda ya
Arusha alipowasili katika viwanja vya Mahakama Kuu-Arusha kukamilisha
ziara yake ya siku mbili mkoani humo.
Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi,
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha,Mhe. Kamugisha akimsomea taarifa ya hali
ya utendaji kazi wa Mahakama katika mkoa huo. Lengo la ziara ya Mhe.
Kaimu Jaji Mkuu katika Kanda hiyo ni kujifunza na kuona hali halisi ya
mazingira ya kazi na utekelezaji wa majukumu.
Naibu Msajili, Mahakama Kuu,
Kanda ya Arusha, Mhe. Rumisha (wa kwanza kulia) akimuonesha Mhe. Kaimu
Jaji Mkuu, moja ya kumbi za Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha pindi
alipokuwa akikagua ofisi mbalimbali za Mahakama ya Mkoa na Mahakama Kuu
katika Kanda hiyo.
Kaimu Jaji Mkuu, Prof. Juma
akiwa katika Kompyuta Mpakato akikagua Mfumo wa Kuratibu takwimu za
Mashauri kwa njia ya Kielektroniki (JSDS) kuhakikisha kama inafanya kazi
ipasavyo, pembeni ni Afisa TEHAMA, Mahakama Kuu-Kanda ya Arusha, Bw.
Athuman
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania,
akiongea na Mahakimu na Watumishi wengine wa Mahakama (hawapo pichani),
katika maongezi yake na Watumishi hao Mhe. Jaji Prof. Juma amewataka na
kuwasisitiza Watumishi hao kufanya kazi kwa kuzingatia Maadili ikiwa ni
pamoja na kuwa na lugha nzuri kwa Wateja/Wananchi wanaowahudumia. kulia
ni Kaimu Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda ya Arusha na kushoto ni Mhe.
Rumisha, Naibu Msajili-Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...