TUMBAKU ni zao ambalo husababisha uharibifu wa Misitu katika uzalishaji wa tumbaku ya Mvuke, kwa kukabiliana na Changamoto hiyo Kampuni ya kuuza na Kununua tumbaku ya Alliance one Wilayani Kasulu imeandaa utaratibu wa kupanda Miti kwa kuwashirikisha Wakulima kutoa Ardhi yao na halmashauri kwa kupanda hekta 288 kwa kila msimu wa kilimo lengo ikiwa ni kuhakikisha kuni zinazotumika katika uchomaji wa tumbaku zinatoka katika chanzo endelevu cha miti wanayoipanda. 

Akizungumza mara baada ya makabidhiano ya Mashamba ya Miti hekta 144 jana yalitooteshwa kwa kipindi cha mwaka 2014 - 2015 katika Kijiji cha Mganza na Chogo kata ya Heru juu baina ya halmashauri na kampuni hiyo Meneja uzalishaji jani katika Kampuni hiyo, David Mayunga, alisema kampuni hiyo inajihusisha na uendelezaji wa nishati mbadara ya kuchomea tumbaku, kuborsha mabani ya kuchomea iliyaweze kutumia kuni chache.

Mayunga alisema uzalishaji wa tumbaku ya Mvuke unategemea kiasi kikubwa cha kuni hapa Tanzania na Nchi nyingine pia na husababisha uteketezaji wa misitu, kampuni hiyo wamedhamilia kuwa ifikapo mwaka 2020 uzalishaji wa tumbaku utatumia kuni kutoka katika vyanzo endelevu ambapo Wakulima na serikali watatoa maeneo yao waweze kupandiwa miti lengo ikiwa ni kuinua uzalishaji wa tumbaku pamoja na Wakulima.

Alisema tumbaku ni zao la pili kwa Tanzania linalo ingiza fedha za kigeni, kampuni hiyo inafanya zoezi hilo katika maeneo ambayo yanalima tumbaku ilikuweza kiwasaidia Wakulima kutunza mazingira na kufanya biashara ya tumbaku bila kiathiri mazingira, kwa kipindi kilicho pita zao la tumbaku limeshuka sana kutokana na Wakulima wengi kushindwa kulima kutokana na gharama ya zao hilo.

"Pamoja na malengo tuliyonayo ya kuinua zoezi la upandaji miti tunakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa Ardhi hili linatokana na baadhi ya Wananchi kuzuia mashamba yao yasipandwe miti kwa kuhofia kwamba watazulumiwa, kukosekana kwa ushirikiano baina ya Viongonzi na kampuni hili linasababisha kampuni kushindwa kupanda miti kwa malengo yaliyo pangwa", alisema Mayunga.
 Meneja wa uzalishaji jani wa kampuni ya Alliance one David Mayunga  akisain hati ya makabidhiano ya mashamba ya  miti kwa Halmashauri ya Wilaya ya kasulu.
Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa kasulu Twallib Mangu, akisaini baadhi ya mikataba ya makabidhiano baina ya kampuni ya Alliance one na halmashauri.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...