KAMPUNI ya kuzalisha makaa ya mawe nchini, Tancoal Energy Limited imetekeleza kwa zaidi ya asilimia 100 agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa ya kuongeza uzalishaji wa makaa ya mawe maradufu.

Taarifa hiyo iliyotolewa jana na Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Bw. James Shedd wakati alipokutana na Waandishi wa habari waliotembelea mgodi huo uliopo eneo la Ngaka katika wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.

Bw. Shedd amesema kwamba, kampuni yake kwa sasa inazalisha kiasi kikubwa cha makaa ya mawe kukidhi mahitaji ya soko la ndani ya tani 60,000 kwa mwezi na ziada ya tani nyingine 20,000 ambazo pia zinauzwa katika nchi za Uganda, Kenya na Rwanda.

“Kampuni yetu imeongeza uzalishaji wa makaa ya mawe kwa zaidi ya asilimia 100 na tayari magari yatumikayo katika ubebaji na uchimbaji wa makaa ya mawe yako njiani kufika huku katika eneo la mgodi ili kuzidi kuongeza uzalishaji na hatimaye tani za uzalishaji wa madini haya zitazidi kuongezeka”, alisema Bw. Shedd.
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Tancoal Energy Tanzania Limited Bw. James Shedd (kushoto) akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu makaa ya mawe katika moja ya ofisi zilizopo katika mgodi wa makaa yam awe wa Liganga uliopo Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma 10 Mei, 2017.
Meneja Udhibiti Ubora wa Makaa ya Mawe wa Kampuni ya Tancoal Energy Tanzania Limited Bw. Bosco Mabena akielezea moja ya majukumu wayafanyayo katika Kitengo cha Udhibiti Ubora wa makaa ya mawe yanayochimbwa kutoka mgodi wa makaa hayo uliopo Ngaka, Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma 10 Mei, 2017.
Kijiko kikifanya kazi ya kuchimba makaa ya mawe katika mgodi wa makaa ya mawe uliopo eneo la mgodi wa Ngaka Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma 10 Mei, 2017.
Malori maalum yakibeba vifusi yakielekea kupakia vifusi vya udongo katika eneo linaloandaliwa kuanza kuchimbwa makaa ya mawe katika eneo la mgodi wa Ngaka Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma 10 Mei, 2017.
Mashine ya kusaga makaa ya mawe katika eneo la mgodi wa makaa ya mawe wa Ngaka Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma ikifanya kazi ya kusaga makaa ya mawe yaliyochimbwa 10 Mei, 2017.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...