Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetaarifiwa kuwa, amri ya kukamatwa kwa Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya jamii Forums, ilitolewa na afisa Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SSP Ramadhan Kindai.
Kauli hiyo imetolewa na yeye mwenyewe SSP Kindai wakati akitoa ushahidi wake mbele ya hakimu Thomas Simba dhidi ya mkurugenzi mtendaji wa Jamii Forum, Maxence Melo na Mwanahisa wa Kampuni hiyo, Mike William.

Shahidi huyo wa kwanza wa upande wa mashtaka amedai, alitoa amri hiyo baada ya washtakiwa kushindwa kutoa taarifa sahihi iliyochapishwa kwenye mtandao wa Jamii Forums..

Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Mohamed Salum, Kindai amedai kuwa waliomba taarifa kutoka kwenye kampuni ya jamii Forums kutokana na kesi iliyofunguliwa na Afisa Msimamizi wa mauzo ya rejareja wa Oil Com, Usama Mohammed.

Ameongeza kuwa Usama alifika kwenye ofisi yao na kulalamika kuwa Februari 13,2016 kuna habari ilichapishwa kwenye mtandao wa Jamii Forums kwamba kampuni ya Oil Com wanakwepa kodi bandari ya Dar es Salaam na kwamba wanaiibia serikali.

Amedai kuwa katika kufuatilia kupata ukweli, ASP Fatuma Kigondo aliingia kwenye mtandao huo kutafuta aliyechapisha taarifa hizo ambapo waligundua kuwa ni Fahara JF Expert member ndiye aliyechapisha taarifa hiyo.
Kufuatia hayo, Februari 23, mwaka Jana Kigondo aliandika barua kwenda kwa Mkurugenzi wa Jamii forums ili awapatie taaarifa za mtu huyo ambapo walipokea barua toka Jamii Forums ikidai kuwa wanahaki ya kulinda faragha za wateja wao.
Pia barua hiyo ilikuwa ikitaka kujua tunaomba taarifa hizo kwa kifungu kipi cha sheria na kwamba Majibu hayo hayakuwa chanya kwa kile walichokiomba.
Aliongeza kuwa, waliandika tena barua Aprili Mosi, 2016 kuwakumbusha Jamii Forums kutoa taarifa walizoziomba sababu kwa mujibu wa kifungu cha 10 (2) Cha Sheria ya Mashauri ya Jinai (CPA) kinawapa mamlaka ya kuomba nyaraka kutoka katika ofisi yoyote na lakini hawakujibu.

Amedai kuwa kutokana na hayo waliona wanakosa haki ya kuendelea na upelelezi, na kuwa wanawadhoofisha katika upelelezi wo ndipo wakaona wawakamate.
Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa kesho. Maxence Melo na Mike William  wanadaiwa kuwa kati ya Aprili Mosi na Desemba 13, mwaka jana, huko Mikocheni wakiwa wakurugenzi wa Mtandao wa Jamii Media Co Ltd ambao unaendesha tovuti ya jamii forums wakijua jeshi la Polisi Tanzania linafanya uchunguzi kuhusiana na mawasiliano ya kimtandao yaliyochapishwa katika tovuti yake kwa njia ya kuuzuia uchunguzi huo walishindwa kutekeleza amri ya kutoa taarifa alizonazo.
Maxence Melo na Mike William wakiwa mahakamani.
BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...