Mwaka 1972, Rais Nyerere aliwaita nyumbani mabalozi wote wa Tanzania waliokuwa nchi za nje kuja kuchukua mafunzo mafupi ya kijeshi kupunguza "nundu" zao baada ya uvamizi wa awali kabisa wa nduli Idi Amin dhidi ya Tanzania. 
Mwishoni mwa mafunzo hayo, mabalozi walipiga picha ya pamoja na wakufunzi wao. Kutoka kushoto walioketi mstari wa mbele: Philip Nhigula, Idris Abdulwakil, Cecil Kallaghe, Ahmed Hassan Diria, mkuu wa mafunzo hayo Gideon Sayore, Chifu Michael Lukumbuzya, Daniel Mloka, Abdalla Sued na Richard Wambura. Mstari wa kati toka kushoto: Anthony Nyaki, Philemon Muro, mkufunzi, Abdul Faraji, mkufunzi, Frederick Rutakyamirwa, mkufunzi, Chifu George Batega Rusimbi na mkufunzi. Mstari wa nyuma toka kushoto: Abbas Kleist Sykes, mkufunzi, Christopher Ngaiza, mkufunzi, Sebastian Chale, wakufunzi wawili, Raphael Lukinda na mkufunzi (Picha kwa hisani kubwa ya Balozi Ngaiza, Rai toleo la Desemba 2001)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...