THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

MAHAKAMA KUU, KANDA YA SONGEA NA KASI YA UONDOSHAJI MASHAURINa Lydia Churi, Mahakama, Songea

Mahakama Kuu, Kanda ya Songea imefanikiwa kwa asilimia 100 kumaliza kesi zote zenye umri unaozidi miaka miwili Mahakamani.

Akitoa taarifa ya hali ya kesi katika Mahakama Kuu, Kanda ya Songea, Jaji Mfawidhi wa Kanda hiyo Mhe. David Mrango alisema hadi kufikia Desemba 2016, Kanda yake ilikuwa na kesi 28 za jinai.

Alifafanua kuwa kesi za jinai zilizofunguliwa kati ya Januari na Mei mwaka huu zilikuwa 51na zilizomalizika na kutolewa hukumu ni 52 na zilizobaki kesi 27.

Kwa upande wa kesi za madai , Jaji Mrango alisema mpaka Desemba 2016, kulikuuwa na kesi 46 za madai kwenye Kanda yake , jumla ya kesi za madai zilizofunguliwa kati ya Januari na Mei 2017ni 42 na zilizosikilizwa na kutolewa hukumu ni 47 wakati zilizobaki ni kesi 41.

Alisema kati ya Januari na Mei, vikao viwili vya kesi za mauaji vilifanyika ambapo kesi 22 zilisikilizwa na 18 zilitolewa hukumu huku 2 zikibaki.

Kuhusu upatikana wa nakala za hukumu, Jaji Mfawidhi huyo alisema licha ya changamoto zilizopo, Kanda yake imekuwa ikitoa nakala za hukumu pamoja na mienendo ya kesi kwa wakati.

Mahakama kuu, Kanda ya Songea ni moja ya Kanda za Mahakama Kuu 13 nchini, Kanda hii ina jumla ya Majaji wawili.