THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Mahakama yawaachia huru wabunge watatu wa Ukawa na Makada wao

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru wabunge watatu wa Ukawa na Makada wao baada ya kuonekana hawana kesi ya kujibu. Wabunge hao na wenzao walikuwa wakikabiliwa na tuhuma za kumjeruhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresa Mmbando.
Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya kiridhika kwamba ushahidi ulioletwa mahakamani hapo haukuwa unatosha kuwakuta washtakiwa na kesi ya kujibu.
Amesema kuwa katika ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka  umeshindwa kuthibisha kwani, hata  mlalamikaji Mmbando hakumbuki ni nani alimjeruhi. Ameongeza kuwa, ushahidi wake ulielezea tu Jinsi washtakiwa walivyojishughulisha na nyaraka siku ya tukio na siyo kumjeruhi.
Kuhusu kushikwa matiti, Hakimu Shaidi alisema kitendo hicho kingeweza kupelekea mlalamikaji kufungua kesi nyingine lakini siyo kujeruhi.

Katika kesi hiyo upande wa mashtaka uliita mashahidi watatu kutoa ushahidi ambapo hakuna ushahidi ulioweza kuwatia hatiani watuhumiwa hao na kukutwa na kesi ya kujibu.
Wabunge wa Chadema, na makada wao pamoja na Wakili Wao Peter Kibatala wakifurahi nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kiachiwa huru kwa kuonekana hawana kesi ya kujibu dhidi ya tuhuma iliyokuwa inawakabili ya kumjeruhi Katibu Tarafa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando. Habari kamili BOFYA HAPA