Na  Bashir  Yakub.

Matunzo  ya  mke  kutoka  kwa  mme  ni  jambo  la  lazima.  Kwa  maana  kuwa  ni  lazima  mme  kutoa  mahitaji  kwa  mke  wake  .Hakuna  uhiari  katika  hili. Ni  lazima  na  neno  lazima  maana  yake inajulikana. Ifahamike  kuwa  matunzo  anayotoa  mme   kwa  mke  wake  si  msaada,  si  hisani, si  upendeleo,  si  zawadi  bali  ni  wajibu.  

Matunzo  yenyewe  ni  kama   chakula ,  sehemu  ya  kulala  na  kuishi, mavazi,  matibabu  na  kila  kitu  ambacho  ni  muhimu  kwa  mahitaji  ya  mke  husika. Kifungu  cha  63(a)  cha  Sheria  ya  ndoa  kinasema  kuwa  ni  wajibu    na  lazima  kwa  mume  kumtolea  matunzo  mke  wake. 

1.VIPI  MUME  AKISHINDWA  KUTOA  MATUMIZI.

Yapo  mambo  ambayo  mke  anaweza  kuyafanya  ikiwa  mme  wake  atashindwa  kumtolea  matumizi .  Mojawapo  ni  hili  la  kuruhusiwa  kuuza  mali  ya  mme  wake  bila  ridhaa  ya  mme huyo. 

Tutaona  likoje  hili  baadae.  Mengine  ambayo  anaweza  kufanya  mke  ikiwa  amenyimwa  matumizi  ni  pamoja  na  kufungua  shauri  mahakamani  kudai  matumizi, na  hata  kudai   talaka  ikiwa  hali  hiyo  imekuwa sugu.

2.  KUUZWA  KWA  MALI  YA   MME.
Kwa  ujumla  kifungu  cha 64( 1 ) cha  Sheria  ya ndoa  kinasema  kuwa  mke  ataruhusiwa  kuuza  mali  ambayo  kimsingi  inamilikiwa  na  mme  wake  kwa  ajili  ya  kujipatia  matunzo  au  mahitaji  muhimu  ya  kwake  na/au   ya  watoto/mtoto  wake. 

Kuhusu  ni  kipi  kinaweza  kuuzwa,  wakati  gani  kiuzwe,  kwa masharti  yapi  tutaona  hapa  chini.
3.  MASHARTI   KABLA  MKE  HAJAUZA.

( a ) Kwanza  ambaye  anaruhusiwa  kuuza  ni  lazima  awe  mke  halali wa  mme  huyo.  Kimada( concubine) hawezi  kuuza  mali  ya  mwenzake.  Ni  mke  wa  ndoa  tu  ndiye  anayeruhusiwa. Yaweza  kuwa  ndoa  ya  kidini, ya  kimila, ya  serikali  au  ile  inayotokana  na kuishi  wote  miaka  miwili.
( b ) Ni  lazima  iwe  mke  amenyimwa  matumizi  muhimu. Ikiwa  hajanyimwa  matumizi  hawezi  kuwa  na  mamlaka  ya  kuuza  mali  ya  mme  wake. 

( c ) Pia  ikiwa  ana  watoto/mtoto  na  hawana  matumizi  basi  napo  anaweza  kuuza  mali  ya  mme  wake.
( d ) Huwezi  kuuza  mali  ya mme  wako   kwa  ajili  ya  kujipatia  matumizi  ya  anasa.  Matumizi  yatakayokupelekea  kuuza  mali  ya  mme  ni  yale  ya  lazima. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...