THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

MAKAMU WA RAIS KUANZA ZIARA YA SIKU TATU MKOANI MARA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, anatarajia kufanya ziara rasmi ya siku tatu kuanzia tarehe 05 Juni, 2017 Mkoani Mara.

Kwa mujibu wa ratiba ya Mkoa, Mhe Samia atatembelea Wilaya ya Tarime, katika Kituo cha Afya cha Nyamwaga kinachojengwa na wananchi kwa msaada wa Mgodi wa Acacia North Mara.

Pia, Mhe. Makamu wa Rais atapata fursa ya kutembelea Bonde la Mto Mara kunakokusudiwa kuanza kilimo cha miwa na ujenzi wa kiwanda cha sukari. Mchana siku hiyo hiyo atafanya mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Bisarwi; katika eneo hilo kunakusudiwa kujengwa kiwanda cha sukari.

Aidha tarehe 6/6/2017 Mhe. Makamu wa Rais ataenda Wilaya ya Serengeti ambapo ataweka jiwe la msingi katika Hospitali ya Wilaya; mchana atafanya Mkutano wa Hadhara katika Uwanja wa Mbuzi, Mugumu mjini.

Tarehe 7/6/2017 Mhe. Makamu wa Rais atakuwa Musoma ambapo ataweka jiwe la msingi kwenye barabara ya km.9.9 inayojengwa kwa kiwango cha lami katika Manispaa ya Musoma. Pia atatembelea kiwanda cha Samaki cha Musoma Fish Processors (T) Ltd na kufanya Mkutano wa Hadhara katika uwanja wa Mukendo Musoma Mjini.

Hii ni mara ya kwanza Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwa na ziara rasmi Mkoani Mara.

Jamal Zuberi
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkoa wa Mara.
30/05/2017