Polisi wanawake kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SARPCO,wakimsikiliza Makamu wa Rais,Samia Suluhu Hassan alipokuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ya siku tatu
Makamu wa Rais Mh.Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya polisi wanawake kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SARPCO,leo katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jijini ,Dar es Salaam.Mh Samia ndiye mgeni rasmi wa mafunzo hayo.Picha na Adam Mzee/VPO.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akishiriki ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya polisi wanawake kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SARPCO,leo katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jijini ,Dar es Salaam.Mh Samia ndiye mgeni rasmi wa mafunzo hayo.Picha na Adam Mzee/VPO.
 Makamu wa Rais Mh.Samia Suluhu Hassan akifuatilia moja ya taarifa wakati wa ufunguzi wa  mafunzo ya siku tatu ya polisi wanawake kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SARPCO.Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere ,Dar es Salaam.Kushoto kwake ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,IGP Ernest Mangu.
Polisi wanawake kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SARPCO wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mafunzo hayo ya siku tatu. 

Makamu wa Rais (wa nne kulia) Mh.Samia Suluhu Hassan akishiriki ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya polisi wanawake kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SARPCO,leo katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jijini ,Dar es Salaam.Mh Samia ndiye mgeni rasmi wa mafunzo hayo.Picha na Adam Mzee/VPO

 Mafunzo ya siku tatu ya polisi wanawake kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SARPCO,yakiendele leo katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jijini ,Dar es Salaam.Mh Samia ndiye mgeni rasmi wa mafunzo hayo.Picha na Adam Mzee/VPO.  
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni wakati wa Mafunzo ya siku tatu ya polisi wanawake kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SARPCO,yakiendele leo katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jijini ,Dar es Salaam.
Baadhi ya Askari wanaoshiriki ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya polisi wanawake kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SARPCO,wakiwasili kwa Gwaride katika.Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere ,Dar es Salaam.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka askari polisi wanawake kutoka kwenye Shirikisho la Majeshi la Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) washiriki kikamilifu katika oparesheni mbalimbali ambazo zinafanyika kwenye ukanda huo kama hatua ya kukabiliana na vitendo vya uhalifu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati akifungua mafunzo ya siku Tatu ya Polisi wanawake kutoka nchi wanachama wa SARPCCO katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewahimiza askari polisi wanawake kufanya kazi kwa bidii na kujituma hatua ambayo itasaidia kupanda vyeo kama  askari wanaume katika maeneo yao ya kazi.Amesisitiza kuwa muda wa kulalamika kuwa hawapandishwi vyeo umeshapitwa na wakati bali kwa sasa wachape kazi na waonyeshe kuwa wanaweza majukumu yao wanayopangiwa ili waweze kupanda vyeo.


“Vyeo haviji tu ni lazima polisi wanawake muonyeshe kuwa mnaweza ili muweze kupandishwa vyeo na kupata nafasi za uongozi katika Majeshi yenu

Kuhusu utendaji kazi wa Polisi wanawake, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka polisi hao kutumia mkutano huo wa siku Tatu kujadili kwa kina namna ya kuondoa changamoto hizo zinazorudisha nyuma utendaji wao wa kazi.


Amesema kama polisi wanawake wataacha majungu na kujenga umoja na mshikamano miongoni mwao watafikia malengo yao haraka hasa katika kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya vitendo vya uhalifu ikiwemo biashara ya dawa za kulevya.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni amesema anaimani kubwa kuwa mafunzo hayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa polisi hao wanawake kuimarika ipasavyo katika utendaji wao wa kazi.
Masauni pia amewahimiza polisi wanawake wanaopata mafunzo hayo kwenda kuwaelimisha na wenzao mipango na mikakati waliyoweka katika kulinda raia na mali zao katika nchi zao.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...