Bw Achiles Bufure, Mkurugenzi Makumbusho
na Nyumba ya Utamaduni Dar es salaam
Leo tarehe
18 May ni siku ya Makumbusho Duniani. Kwa hapa Tanzania, Makumbusho na Nyumba
ya Utamaduni itaungana na Makumbusho zote duniani katika kuadhimisha siku hii muhimu. Hivyo watanzania wameshauriwa kuhudhuria kwa wingi katika maadhimisho hayo ili waweze
kupanua uwelewa zaidi wa mambo mbali mbali yanayo huyu maisha yao na nchi kwa
ujumla.
Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar Es Salaam
Bwana Achiles Bufure akiongea ofisini kwake ameongeza kuwa katika
Maadhimisho hayo, kutakuwa na Onesho maalum litakaloonesha vifaa mbali mbali
vya ofisi alivyotumia Muasisi wa Taifa hili Baba wa Taifa Mwalimu
Julias Kambarage Nyerere, pamoja na mafunzo shirikishi kwa watoto juu ya shughuli za
kimakumbusho na Onesho la jukwaani.
Wananchi
mbali mbali wameisifu Mkumbusho na Nyumba ya Utamaduni kwa kuadhimisha siku
hiyo kwa kufungua milango hata kwa watu wasio na uwezo wakulipia pindi wanapo
tembelea Makumbusho hiyo kwakuwa na wao watapata nafasi adhimu ya kujifunza
mambo yanayo husu nchi yao kwa kupitia vioneshwa vilivyopo ndani ya Makumbusho.
Maadhimisho hayo ya Siku ya Makumbusho Duniani
yatadumu kwa muda wa wiki moja kuanzia leo ili kutoa nafasi kwa watanzania
warika mbali mbali kutembelea Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni na kwa tarehe
18 May hakutakuwa na kiingilie cha kuingia na kutembelea maonesho mbalimbali
yaliyopo Makumbusho hiyo iliyopo mkabala na chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM)
Dar es Salaam, Posta.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...