Na.Vero Igantus.Arusha

Mamlaka ya usimamizi wa Bima nchini(TIRA)imezindua mfumo wa uhakiki wa Bima kwa njia ya simu za mkononi kanda ya Kaskazini ambapo zoezi hilo limeambatana na ukaguzi wa bima kwenye vyombo vya moto na kubaini bima feki katika baadhi ya magari na pikipiki.

Akizindua mfumo huo kwa kanda ya kaskazini uliofanyika jijini Arusha Kamishna wa Bima Nchini Dkt.Boghayo Saqware amesema kuwa kampeni yao ina laengo la kuondoa bima feki sokoni ambazo zinazouzwa ama kutengenezwa na wahalifu ,ambalo kwa mujibu wa sheria wanafanya kosa la jinai.

“Tumeanzia Pwani na sasa tupo Arusha na zoezi hili litakuwa endelevu,kwahiyo tunawaasa wananchi wanunue bima halali,tumezindua mfumo ambao ni rahisi kwa mtu anaenunua bima kujihakikishia kuwa bima hiyo ni feki au halali .”alisema Dkt.Boghayo.

Kamishna huyo amesema kuwa kwa miaka( 3) kesi (10) za Bima feki ziliamuliwa ,watu(5) walihukumiwa kifungo jela,(2) wamelipa bilioni 20,000,000, hadi 40,000,000,mashauri ya jinai yaliyopo mahakamani yalifunguliwa mwaka 2016 Mbeya(1) Mafinga(2) Mara(1) na Dar es salaam (3) na kufikia jumla ya kesi mpya 7,ambapo mashauri yaliyopo kwenye uchunguzi wa polisi ni (10).

Kwa upande upande wake Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Kanda ya kaskazini Eliezer Rwekiza amesema kuwa zoezi hilo katika Jiji la Arusha litaendelea kwa wiki nzima ambapo wataelekea Kilimanjaro ,Tanga ambapo amesema kuwa 10% ya magari hapa nchini Tanzania hayana Bima halali,amesema hadi sasa hapa nchini kuna makampuni 31 ya Bima,mawakala 500 madalaliwa Bima ni zaidi ya 100.

Kaishna wa Bima nchini Dkt.Boghayo Saqware akiwa anazungumza na wauza bima,madalali wa bima,mawakala wabima,wauza bima,jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani, viongozi wa vyama vya wamiliki wa mabasi pamoja na umoja wa waendesha pikipiki.Picha na Vero Ignatus Blog.
Meneja wa Mamlaka ya usimamizi wa Bima (TIRA)Kanda ya kaskazini Eliezer Rwekiza akizugumza katika uzinduzi huo wa uhakiki wa Bima kwa njia ya simu ya mkononi,uliofanyika Jijini Arusha leo,wa kwanza kulia ni Kamisha wa Bima Taifa Dkt.Boghayo Saqware,akifuatiwa na aliyepo kulia kwake ni Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Nuru Suleiman

Meneja waTEHEMA kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA)Aron Mlaki akiwa anawonyesha namna ya kutambua Bima kama ni halali au ni feki kwa kutumia simu ya mkononi .Picha na Vero Ignatus Blog.
Mkurugenzi wa masoko kutoka Mamlaka ya usimamizi wa Bima (TIRA) Bi.Adelaida Muganyizi akiwa anazungumza na wauza bima,madalali wa bima,mawakala wabima,wauza bima,jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani, viongozi wa vyama vya wamiliki wa mabasi pamoja na umoja wa waendesha pikipiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...