Na Ismail Ngayonga, MAELEZO

KATIKA  kipindi cha Mwaka wa Fedha wa 2015/16,  Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) ilifanya ukaguzi wa manunuzi ya umma na uhakiki wa ukaguzi uliofanyika Mwaka wa Fedha 2014/15.

Ukaguzi huo ulilenga kuangalia iwapo mikataba ya manunuzi iliyoingiwa katika kipindi husika ilitekelezwa au inatekelezwa kwa mujibu wa vigezo na masharti yaliyoainishwa kwenye mikataba husika inalingana na thamani ya fedha za umma zilizotumika. 

Katika ukaguzi wa uhakiki wa mwaka 2014/15, jumla ya ya taasisi nunuzi 70 zilifanyiwa ukaguzi wa ukidhi uliongalia namna taasisi hizo zilivyozingatia sheria na kanuni za manunuzi pamoja na matumizi ya nyaraka za miongozo na mifumo iliyoandaliwa na PPRA. 

Taasisi zilizoguswa na ukaguzi huo uliofanyika kati ya mwezi Aprili na Septemba, 2016 ni pamoja na taasisi 15 zilizo kwenye kundi la Wizara, Idara na Wakala za Serikali, Mamlaka za Serikali za Mitaa 25; na mashirika ya umma 30.

Jumla ya mikataba 21,313 ya manunuzi yenye thamani ya Tsh Trilioni 1.05 ilifanyiwa ukaguzi huo, ambapo kati yao mikataba 118 yenye thamani ya Tsh. Bilioni 55.34 ilikaguliwa katika halmashauri za serikali za mitaa.

Aidha taarifa hiyo inaongeza kuwa katika mikataba 122 ya ukusanyaji wa mapato iliyokaguliwa katika Malmaka tisa za Serikali za Mitaa, kumebainika mapungufu kadhaa katika usimamizi wa mikataba hiyo ambapo kumesababisha halmashauri hizo kushindwa kukusanya kiasi cha shilingi 761.54 milioni.

Inaelezwa kuwa pamoja na hasara hiyo, ukaguzi unaonesha kuwa halmashauri hizo hazikuchukua hatua zozote dhidi ya wazabuni waliopewa jukumu hilo kwa mujibu wa mikataba waliyoiingia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...