THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MAONYESHO YA SITA YA MADINI YA VITO YAANZA RASMI LEO JIJIJI ARUSHA

Na Woinde shizza, Arusha
Maonesho ya sita ya madini na vito maarufua kama Arusha Gem fair yameanza rasmi jijini Arusha leo huku ikielezwa kwamba Wananchi wengi wanaoishi karibu na migodi inayochimbwa madini ya aina mbalimbali wamekuwa hawanufaiki kutokana na viongozi wa maeneo husika kutokuwa na mahusiano mazuri na wamiliki wa migodi hiyo.
Hayo yamebainishwa na Mbunge wa jimbo la Simanjiro Mhe. James Ole Milya wakati akiongea katika uzinduzi wa maonesho hayo. 

“Asilimia kubwa ya wananchi ambako madini hayo yanachimbwa ukifuatilia maisha yao ni duni na hawana maendeleo yoyote. Kwa ufupi hawanufaiki na madini ambayo yanatoka katika maeneo yao. Hivyo ni wajibu wa Serikali kuangalia upya sera ya madini.

"Mfano mwananchi wa Mererani madini yanachimbwa kwao, lakini ukiangalia maisha wanaoyoishi huwezi kusema wanakaa sehemu inayotoka Tanzanite ambako ni hapo pekee duniani,”alisema Milya
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Madini katika Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe amesema kuwa sera ipo na sheria zipo za kuhakikisha wananchi ambao wanazunguka maeneo ya migodi wananufaika na migodi hiyo, lakini ukifuatilia kwa kiasi kikubwa wale wananchi ambao hawanufaiki ni wale ambao unakuta viongozi wao wa mtaa au kijiji hawana ushirikiano mzuri na viongozi au wawekezaji waliowekeza katika maeneo yao.
"Hivyo ni wajibu wa wananchi pamoja na viongozi kushirikiana kwa pamoja na kuungana ili kuweza kusaidia", alisema.
Bw. Mdoe aliongezea kuwa haya ni maonyesho ya sita kufanyika na yanafanyika kwa muda wa siku tatu, lengo ikiwa ni kutimiza dira iliopo katika sera ya madini ya mwaka 2009 inayosisitiza kuwa Tanzania iwe kitovu cha madini.
"Sekta ndogo ya vito inachangia katika uchumi wa maendeleo ya jamii hivyo maonyesho haya ni fursa kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa hapa nchini kuweza kupata fursa ya kujitangaza zaidi.
“Wageni wengi kutoka nchi mbalimbali wanahudhuria katika maonyesho haya, wengine wanakuja kununua madini wengine wameleta madini yao ili yauzwe> kwa hiyo hii ni fursa ya pekee ya wachimbaji wetu wa ndani kujitangaza na kupanua soko la zaidi kikubwa zaidi waangalie ni namna gani watayafanya madini yao yawe na dhamani zaidi”alisema Bw. Mdoe.
baadhi ya madini yaliyoletwa katika maonyesho
Mkuu wa mkoa wa Manyara Dk Joel Bendera akifuatilia jambo wakati alipokuwa anazindua rasmi maonyesho ya sita ya vito na madini yanayofanyika katika hotel ya Mounti Meru ilipo jijini Arusha.
Meya wa jiji la Arusha Mstahiki Calist Lazaro pamoja na wabunge kadhaa aalihudhuria katika uzinduzi wa maonyesho hayo ya vito na madini.
Habari picha na Woinde Shizza, Arusha.


Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

  1. Mr. Ally Anasema:

    Hii kusema viongozi hawana uhusiano na wachimba migodi ni siasa zilizopitwa na wakati. Mali hiyo ni ya wananchi hata aje achimbe nani. Serikali inatakiwa kuhakiki mali yote inayotoka migodini na kodi kiasi lazima iende kwa wananchi wa mahala pale. Nyerere alikataa kuchimba mpaka watu wapate elimu. Sasa kwa sababu wananchi wengi bado hawajui haki zao madini yanaibwa tu. Hii mbaya sana!