Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

Mashindano yanayoitwa European Youth Film Competition yamezinduliwa rasmi leo, May 29, 2017 ambapo yatafanyika nchini Tanzania kwa mara ya kwanza.

Mashindano hayo yameandaliwa na Umoja wa Ulaya (EU) na washirika nchi za Netherlands, United Kingdom, Ubalozi wa Ufaransa, Alliance Française, British Councils pamoja na Bodi ya Filamu nchini Tanzania.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Afisa Habari wa Umoja wa Ulaya (EU), Susanne Mbise amesema katika shindano hilo vijana watapata fursa ya kuzungumzia mijadala ya maendeleo wakati watakapokuwa wakizungumzia Suala la Ongezeko la idadi ya watu nchini Tanzania, Afrika na Duniani. Swali likiwa Je suala hilo ni changamoto au fursa ya maendeleo?

"Ndani ya Filamu za dakika 5 au 10 Washiriki wanatakiwa kuandaa Filamu ya aina yoyote, iwe 'Documentary', Maigizo lakini iwe dakika 5 au 10 katika Maudhui hayo", amesema Mbise.

Mbise amesema kuwa Kati ya vijana hao wenye umri kati ya miaka 18-35 watashindana na Washindi wa tano bora watakwenda kwenye Mashindano makubwa.

Kwa upande wa Bodi ya Filamu nchini, Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa Bodi hiyo, Abuu Kimario amewapongeza Umoja wa Ulaya kwa kuandaa Mashindano hayo, kwani yamekuja siku muafaka, kutokana na Soko la Filamu linapanda na kushuka.

Naye Mratibu wa Mashindano hayo, Moses Saka amesema kuwa mshindi wa kwanza katika Shindano hilo atazawadiwa kiasi cha Shilingi Milioni 7, mshindi wa pili Sh. Milioni 5, na mshindi wa tatu Sh. Milioni 3 za Kitanzania.
 Afisa Habari wa Umoja wa Ulaya (EU), Sussane Mbise (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mashindano ya European Youth Film Competition (EYFM) yanayozinduliwa May 29. Kulia ni Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa Bodi ya Filamu nchini, Abuu Kimario, Kushoto ni Mratibu wa Shindano hilo, Moses Sakar. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...