Na Mwandishi Wetu, Pwani

BAADHI ya wananchi wilayani Kibiti, mkoani Pwani, wamewataka viongozi wa vyama vya siasa vikubwa wilayani humo kukaa meza moja kuangalia namna ya kukemea vitendo vya mauaji vinavyoendelea kwenye ukanda huo.

Aidha wamesema kwa umoja wao kutawezesha kushirikiana na serikali kumaliza janga hilo. Pia wameiomba serikali kupeleka askari wa JWTZ kutanda katika wilaya za Rufiji na Kibiti hadi maeneo ya vijijini ili kudhibiti vitendo hivyo vinavyomaliza watu wasio na hatia.

Hata hivyo, wameitaka serikali kuwadhibiti wahamiaji haramu wanaoingia kwenye njia za panya zilizopo Pwani kwani yawezekana baadhi yao wanaweza kuhusika katika matukio hayo.
 Hadija Issa, Hamis Kidongezo na Seif Mohammed waliyasema hayo, baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba na Mkuu wa Mkoa huo Mhandisi Evarist Ndikilo, kwenda kuzungumza na wananchi katika maeneo hayo.

Walieleza, CCM na CUF taifa, mkoa na wilaya wanapaswa kutupia macho suala hilo kwa upana ili kubaini chanzo halisi kinachosababisha wauawe.

Hadija alisema, inashangaza vifo vinavyoendelea kutokea wanakufa sana viongozi wa chama fulani lakini wapo viongozi wa vyama vingine wamenyamaza kama vile hakuna kinachoendelea.

Alisema serikali na askari polisi wanafanyakazi nzuri lakini inabidi kujulikane kina cha tatizo.


Hadija alieleza ,ugaidi unaweza ukawepo lakini anadhani pia kuna chembe ya masuala ya kisiasa ."Yaani sidhani km vyama vingine vingepigwa kiasi hicho ingekuwaje, Naona kuna haja ya vyama vyote vikaguswa na hili, maana hii agenda lisingekuwepo bunge ina maana viongozi wa vyama vingine vinavyokuwa na sauti kubwa ya kutetea mengi wasingeongeaa"


"Tunaomba wanasiasa na wanaharakati wapige kelele kwa hili kama ilivyo katika mambo mengine ya kijamii wanavyofanya" alisema Hadija .

Hamis alielezea kwamba, bado wananchi ambao ni wanachama na viongozi wa CCM, wanashindwa kuvaa sare za chama na kuogopa kuitana majina ya vyeo vyao.

Seif, alisema baadhi ya viongozi wa vijiji na vitongoji wanashindwa kwenda ofisini kutekeleza majukumu yao. Alisema wanaishi kwa sintofahamu na imani inawatoweka, watu wanakiogopa chama kwasasa na kukimbia miji, ofisi na kushindwa kuchukua fomu kugombea nafasi za ndani 

Anaeleza miaka ya nyuma watu walikuwa wakigombea nafasi mbalimbali za uongozi lakini kwa sasa wanakwepa na kuhofia uhai wao.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...