KIKOSI Mbeya City Fc , leo kimeanza safari kuelekea jijini Dar es Salaam tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya wenyeji Yanga uliopangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Taifa mwishoni mwa wiki hii. 

Afisa habari wa kikosi hicho Dismas Ten amesema kuwa jumla ya nyota 18 na viongozi 10 watakuwa kwenye msafara huo kwa ajili ya kuhakikisha City inafanikiwa kuibuka na pointi tatu muhimu na kujiweka kwenye mazingira mazuri katika msimamo wa ligi. 

Ligi iko kwenye hatua za mwisho, huu ni mchezo muhimu na matarajio yao ni kushinda na kupata matokeo muhimu kwenye mchezo wa jumamosi, kwani wanafahamu Yanga ni timu nzuri na iko kwenye mbio za ubingwa lakini hilo haliwapi hofu kwa sababu wana kikosi kizuri. 


Ten amesema katika duru ya kwanza waliweza kupata matokeo mazuri na sasa wanakwenda Jijini Dar kuhitimisha dhamira yao ya kupata pointi sita msimu huu kutoka kwao

Akiendelea zaidi Ten alisema City imekuwa na wiki nne za kujindaa vizuri ili kuikubali Yanga kwa kufanya mazoezi mazito ikiwa ni pamoja na kucheza michezo zaidi ya mitano ya kirafiki ambayo imesaidia kuimarisha uwezo wa nyota wa kikosi kiuchezaji na kuwaongezea Morari ya kutaka kushinda kwenye uwanja wa Uhuru. 

"Tumekuwa na wiki nne za kujindaa, hatukucheza mchezo wowote baada ya sare ya 1-1 na African Lyon kwenye uwanja wa Sokoine April 13,hivyo nguvu zetu zote tunaziweka siku ya jumamosi kwenye uwanja wa Taifa,".amesema Ten. 

Miongoni mwa nyota waliopo kwenye msafara huo ni pamoja na Mrisho Ngassa,Hassan Mwasapile,Tumba Lui na Zahoro Pazzi 

Kwa upande wake kocha mkuu Kinnah Phiri amesema hana wasiwasi na mchezo huo wa jumamosi kwa sababu anaifahamu vyema Yanga hasa baada ya kuifuatilia kwenye michezo kadhaa na tayari ameandaa mbinu za kuhakikisha vijana wake wanapata ushindi. 

"Sina wasiwasi,wakati huu ambao sikuwa na mchezo wa ligi nilikuwa nawafuatilia, najua mbinu zao na nimewandaa vijana wangu vizuri ni wazi tutashinda tena dhidi yao kama ilivyokuwa kwenye mchezo wa duru ya kwanza".

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...