THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MBUNGE AZZA HAMAD ATOA MSAADA WA VIFAA TIBA VITUO VINNE VYA AFYA KISHAPU SHINYANGA


Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad Jumamosi Mei 6,2017 amekabidhi Vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 12.6 katika vituo vya afya vinne vya afya ambavyo ni Nhobola, Songwa, Ng’wang’haranga na Dulisi vilivyopo wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.
Hapa ni ndani ya kituo cha afya Nhobola wilayani Kishapu ambapo Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (wa pili kushoto) akisikiliza maelezo ya Mganga mkuu wa Kituo cha afya Nhobola kilichopo kata ya Talaga,Bhujiku Mganga Nyanda
Mganga mkuu wa Kituo cha afya Nhobola Bhujiku Mganga Nyanda akieleza jinsi akina mama wajawazito walivyokuwa wanapata changamoto wakati wa kupata matibabu
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akiwa katika wodi ya wazazi amebeba mtoto wa mkazi wa Kata ya Talaga baada ya kujifungua katika kituo cha afya cha Nhobola.