Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ametoa msaada wa vifaa tiba ikiwemo vitanda vya kisasa vya kujifungulia,vitanda vya wagonjwa na viti vya wagonjwa katika vituo vya afya na zahanati katika halmashauri ya Shinyanga vijijini na Kishapu vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 33.

 Mbunge huyo amekabidhi vifaa tiba hivyo katika Kituo cha afya Tinde,zahanati ya Solwa,zahanati ya Nyashimbi,kituo cha afya Samuye katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini na kwa upande wa Kishapu ni Kituo cha afya Nhobola,Mwang’haranga,Dulusi na Songwa.
  
Vifaa hivyo vinatokana na jitihada zilizofanywa na mbunge huyo Azza Hilal Hamad kufika katika ubalozi wa China nchini Tanzania kuomba asaidiwe vifaa tiba hivyo ili kukabiliana na vifo vya mama na mtoto mkoani Shinyanga.

Akizungumza leo Jumamosi May 13,2017 wakati wa kukabidhi vitanda vitatu vya kisasa vya kujifungulia,vitanda 9 vya wagonjwa na viti vitatu (wheel chairs) vyenye thamani ya shilingi milioni 9.7 katika kituo cha afya Tinde kilichopo Shinyanga vijijini,mheshimiwa Hamad alisema vitasaidia kupunguza adha ya upungufu wa vitanda katika kituo hicho kilichojengwa mwaka 1920.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)  akimkabidhi Mganga Mkuu wa kituo cha afya Tinde,Dkt. Dama s Mnyaga Nyansira,shuka kwa ajili ya vitanda vya kulalia wagonjwa
 Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwahutubia wakazi wa kata ya Tinde wakati akikabidhi vifaa tiba hivyo 
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) akipokelewa kwa shangwe katika kituo cha afya Tinde kilichopo Shinyanga vijijini alipofika kukabidhi vitanda vya kisasa na viti vya wagonjwa vyenye thamani ya shilingi milioni 9.7

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...