Nuru Juma – MAELEZO.

Serikali imeipongeza Bodi na Menejimenti nzima ya Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) kwa juhudi zao zakurejesha uhai wa Shirika hilo richa ya changamoto wanazo kumbana nazo.

Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR –TAMISEMI), George Simbachawene wakati akipokea taarifa fupi ya Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) na Shirika la Masoko Kariakoo alipokutana na menejinti ya mashirika hayo leo.

Waziri Simbachawene alisema kuwa amepitia taarifa ya Shirika hilo na kuridhika nayo hivyo hana budi kuipongeza timu nzima ya uongozi kwani kwa muda mfupi imeweza kufanya mabadiliko na kuweza kuliinua tena Shirika hilo.

“Pamoja na kuipongeza bodi hii lakini napenda kuwashauri kuangalia maeneo mengine ya kuwekeza kama kufungua maeneo mengi zaidi ya burudani kwani hilo ndilo lilikuwa lengo la kuanzishwa kwa DDC,ikiwa ni pamoja na kuweka mahali ambapo watoto wataweza kucheza ili kuhakikisha shirika linajiongezea kipato na kuiongezea Serikali kipato pia,” alisema Waziri Simbachawene.

Simbachawene alitumia nafasi hiyo kuwaagiza Wakuu wa Mashirika ya Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam kuhakikisha wanaandaa taarifa nyingine itakayohusisha mali zote za mashirika hayo.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George Simbachaweni akipokelewa na wafanyakazi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam alipokuwa katika ziara ya kikazi kutembelea Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC).Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam  Sipora Liana na Mstahiki Meya wa Jiji hilo Isaya Mwita.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George Simbachaweni akizungumza na menejimenti za Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) wakati wa ziara yake katika ofisi za mashirika hayo leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Masoko Kariakoo Dkt. Hoseana Bohela Lunogelo.
Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Bi. Sipora Liana akifafanua jambo wa mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) George Simbachawene (mbele) alipokuwa katika ziara ya kikazi kutembelea Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) leo.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akisisitiza jambo mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) George Simbachawene (kulia) wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo katika Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) leo.Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Masoko Kariakoo Dkt. Hoseana Bohela Lunogelo

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...