THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Meno ya tembo yamtupa jela miaka 20

Na Karama Kenyunko- blogu ya jamii.

Mkulima mmoja Samwel Nicodem Bwandu 38, amehukumiwa kwenda jela miaka 20 baada kupatikana na hatia ya kukutwa na vipande nane vya meno ya tembo vyenye thamani ya milioni 60.

Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Akisoma Hukumu, huyo hakimu shahidi amesema kuwa, upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha mashtaka bila ya kuacha shaka kuwa kweli Bwandu alikutwa na meno ya tembo lakini haukuweza kuthibitisha kuwa alikuwa akijihusisha na biashara hiyo.

Hata hivyo, mahakama hiyo,imemuachia huru Kidamisi Kidarageda Kidiwami, Mkazi wa Iringa baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake kuwa alihusika katika tuhuma hizo za meno ya tembo.

Watuhumiwa wote wawili, Bwandu na Kidawami walikuwa wakituhumiwa kwa makosa ya kupatikana na nyara za serikali ambazo ni vipande nane vya meno ya tembo vyenye thamank ya milioni 600 na Kijihusisha na nyara hizo zenye thamani ya milioni 900.

Hakimu Shahidi amesema, amezingatia ushahidi wote uliotolewa na upande wa mashtaka na utetezi wa washtakiwa na kuridhika kwamba mshtakiwa Kidawami hakuhusika katika kutenda makosa hayo.

"Hakuna shahidi yeyote aliyefika mahakamani hapo na kuthibitisha kuwa mshtakiwa wa Kidawami alihusika na tuhuma hizo, isipokuwa shahidi namba tano ambaye nae alikuwa na ushahidi wa kusikia tu", amesema hakimu Shahidi"