Mfuko wa Pensheni wa PPF umeendelea kukabidhi vifaa tiba katika hospitali na vituo vya afya nchini kulingana na sera yake ya uchangiaji na udhamini. 
 
Katika wilaya ya Kisarawe, Mfuko wa PPF umekabidhi vifaa tiba hivyo kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI,Utumishi na Utawala bora Mhe. Selemani Jaffo kwa ajili ya hospitali ya Wilaya ya Kisarawe ambavyo ni vitanda 2 vya kujifungulia wakinamama, vitanda 4 vya wagonjwa wa kawaida, mashuka 56 na vifaa vinavyotumika kujifungulia wakinamama. Akipokea vifaa hivyo, Mhe. Jaffo alisema Mfuko wa PPF walichofanya ni jambo kubwa kwa vile hospitali za wilaya ya Kisarawe zilikuwa zikikabiliwa na changamoto katika sekta ya afya. 
 
Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele, alisema Mfuko umetoa vifaa tiba hivyo ikiwa ni muendelezo wa zoezi la kurudisha kwenye jamii kulingana na sera ya uchangiaji na udhamini ya PPF. Alisema Kisarawe ni wilaya ya nne kupata vifaa hivyo na kwamba wataendelea kutoa kwenye hospitali nyingine 12 nchini. 
 
Lulu alisema Mfuko wa PPF, umetoa vifaa tiba vyenye jumla thamani ya Sh. 99,983,700/-. Shughuli hiyo ya kukabidhi vifaa tiba kutoka Mfuko wa PPF ilienda sambasamba na taarifa ya kukabidhi vifaa tiba kutoka kwa Mfamasia Mfawadhi wa Ofisi ya Rais (TAMISEMI),Regina Joseph kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Utumishi na Utawala bora Mhe. Selemani Jafo, alisema kuwa Rais Dkt. Magufuli ametoa vitanda 20 vya kulalia, vitanda sita vya kujifunguli. Vifaa kama hivyo vinasambazwa katika hospitali nyingine nchi nzima. Naibu wa Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Utumishi na Utawala Bora, Seleman Jaffo akipokea msaada wa vifaa tiba kutoka Meneja Uhusiano wa Mfuko wa PPF, Lulu Mengele wakati wa halfa ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika jana katika hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Pwani.
Naibu wa Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoaa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Utumishi na Utawala Bora, Seleman Jaffo akimkabidhi vifaa tiba kwa Mganga mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Elizabeth Oming'o kwa ajili ya hospitali ya wilaya ya Kisarawe.

Vifaa tiba vilivyotolewa na Mfuko wa PPF.
Naibu wa Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoaa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Utumishi na Utawala Bora, Seleman Jaffo (wa tano toka kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness Nedesa wakiwa katika picha ya pamoja baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa PPF na wafanyakazi wa wilaya ya Kisarawe. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...