MKAZI wa Bunju jijini Dar es Salaam, James Peter amefanikiwa kuibuka kidedea katika droo ya tano ya wiki ya kuwania Sh Milioni 10 baada ya kutangazwa mshindi kwenye kinyang’anyiro hicho.

Droo hiyo ya tano ya wiki imechezeshwa leo jijini Dar es Salaam na Balozi wa Biko, Kajala Masanja kwa kushirikiana na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Emmanuel Ndaki.

Akizungumza katika droo hiyo ya tano, Kajala Masanja alisema mshindi wa Milioni 10 wa wiki hii alibahatika kutangazwa mshindi baada ya kupigiwa simu mara tatu, huku mara mbili akishindwa kupokea simu kwa haraka.

Alisema hata hivyo baadaye alipokea simu hali inayoonyesha kwamba alikuwa na bahati kubwa kwa kunyakua fedha hizo zinazotolewa kwa mshindi mmoja kila mwisho wa wiki, huku washindi wengine zaidi ya 20,000 wa zawadi za papo kwa hapo wakijishindia zawadi kem kem.

“Tumefanikiwa kumpata mshindi wa Sh Milioni 10 ambaye anatokea jijini Dar es Salaam, akiongeza idadi ya washindi wanne kutokea jijini hapa, huku mmoja pekee akitokea jijini Mwanza,” alisema Kajala.

Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven aliwataka Watanzania hususan wakazi na wananchi wa mikoa mbalimbali ya Tanzania kujitokeza kwa wingi kucheza biko ili waibuke washindi kwa kufanya miamala kwenye simu zao za Tigo, Vodacom na Airtel ambapo katika kipengele cha lipa bili wataingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 na namba ya kumbukumbu 2456.

“Kucheza biko ni rahisi kwa saabubu baada ya kuweka kiasi kuanzia Sh 1000 ambayo inatoa ushindi wa papo kwa hapo pia humpa fursa mtu kuingia kwenye droo kubwa ya wiki ya kuwania Sh Milioni 10, huku zawadi za papo kwa hapo zinatolewa na Biko ikianzia sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja, huku hadi sasa washindi zaidi ya 20,000 wakiwa wamenyakua zawadi mbalimbali za fedha kutoka kwetu Biko,” Alisema.

Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akiagana na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Emmanuel Ndaki baada ya kumaliza kuchezesha droo ya tano ya Sh Milioni 10 ambapo mkazi wa Bunju, jijini Dar es Salaam, James Peter kutangazwa mshindi wa droo hiyo ambapo amejishindia jumla ya Sh Milioni 10.
Balozi wa Biko Tanzania Kajala Masanja akifurahia namba ya ushindi ambapo mkazi wa Bunju, jijini Dar es Salaam, James Peter amejinyakulia jumla ya Sh Milioni 10 katika droo iliyochezeshwa jana jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Emmanuel Ndaki. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...