Na
Bashir Yakub.
Ndio ni kweli
mwanamke aliyeolewa anaweza
kukopa hela kwa
jina la mme
wake. Tena kukopa
kwenyewe si lazima
awe amepata ridhaa
au ruhusa kutoka
kwa mme wake.
Pia si ruhusa tu
bali si lazima
amtaarifu mme huyo. Sheria
ya ndoa , sura
ya 20 iliyofanyiwa
marekebisho mwaka 2010
ndiyo iliyoeleza jambo hili . Lipo kifungu cha
64 cha sheria
hiyo.
Kwa ujumla makala
haya yatatizama jambo
hili likoje, linahusisha nini na
nini, vigezo na sifa
za kufanya hivyo na
mambo mengine ambayo
yanalizunguka jambo hili
lakini kwa ufupi.
1.MWANAMKE GANI
ANAWEZA KUKOPA.
Kifungu hicho kimesema mwanamke anayeweza
kukopa ni yule
aliye kwenye ndoa
inayotambulika kisheria. Ikiwa
mwanamke hayupo katika ndoa
ambayo sheria inaitambua basi
haki hii ya
kukopa kwa jina
la mme wake
anaikosa.
Ikiwa mmetengana lakini
ndoa haijavunjika kisheria
basi haki hii inaendelea kubaki.
Isipokuwa tu itaondoka
ikiwa mmetengana kwa
makubaliano maalum ambapo
matunzo na matumizi
yote mwanamke anapata
bila wasiwasi.
Pia ikiwa kuna
talaka basi mwanamke
hawezi kukopa kwa
jina la mme
wake kwa kuwa
talaka kisheria inavunja
ndoa na hivyo
tafsiri yake ni kuwa
hakuna ndoa. Lakini
kukiwa na shauri
la talaka mahakamani
na ndoa haijavunjwa
rasmi na mahakama
basi haki hii
inaendelea kubaki kwa
mwanamke huyo.
2. KWANINI SHERIA
IMEMRUHUSU MWANAMKE KUKOPA
KWA JINA LA
MME .
Sheria imemruhusu mwanamke
kukopa kwa jina
la mme wake tena
bila hata ridhaa
ya mme wake
kwakuwa imempa wajibu
mume kumtunza mke
wake na mtoto/watoto
kama yupo. Kwa
mujibu wa sheria
ya ndoa ni
lazima mume kumtunza
mke wake pamoja
na watoto kama wapo.
Kwa upande mwingine
mwanamke naye anaruhusiwa
kumtunza mme wake
lakini kwake sio
lazima. Sheria haijampa
ulazima mwanamke bali
mwanaume . Kwahiyo ni
katika mazingira haya
ambapo suala la mke
kukopa bila ridhaa
ya mme wake
tena kwa jina
la mme huyo
linapokuja.
Hata hivyo sio
wakati wote mwanamke
anaruhusiwa kukopa kwa
njia hiyo bali
ni pale tu mume
wake anapokaidi wajibu
wake wa lazima
wa kumpa matunzo/matumizi. Hapa
ndipo mwanamke anaweza
kukopa kwa jina
la mme wake
tena bila hata ridhaa ya
mme huyo.
Mke hataruhusiwa
tu kufanya hivyo
kwa kutopewa mahitaji
yake pekee bali pia
hata kama ana watoto/mtoto nao
hawajapewa mahitaji basi
hata hapo anaruhusiwa
kukopa.
KUSOMA ZAIDI
sheriayakub.blogspot.com
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...