Mkuu wa wilaya Iringa Mhe Richard Kasesela leo amefanya ziara ya kukagua madarasa na mabweni katika shule ya sekondari Tagamenda ikiwa ni maandalizi ya kupokea kidato cha 5 mwezi wa 7. Katika ziara yake aliyo ambatana na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Bwana Omar Mkangaa, Mhe Kasesela aliagiza kasi ya ujenzi wa madarasa hayo na mabweni iongezeke ikiwezekana wajenge hata usiku ili tuweze kupokea wanafunzi wa kidato cha 5, huku akisisitiza kwamba mpaka sasa fedha za ujenzi zimeishapatikana kinachotakiwa ni kasi ya ujenzi. 

Kwa sasa shule ya sekondari ya Tagamenda ina wanafunzi 882 wakiwemo wasichana 503 na wavulana 379. Inatarajia kupokea wasischana 120 kidato cha tano. Ujenzi wa madarasa 4 kwa thamani ya shilingi milioni 80, mpaka sasa kiwanja kimoja kipo katika hatua ya kupaka rangi na vyumba 3 na ofisi ya mwalimu vipo katika hatua ya kupiga kenchi. Akitoa taarifa fundi mjenzi Bwana Emmanuel Mhelamvi alisema mpaka sasa kiasi cha shilingi 56,447,102.40 zimekwisha tumika bado shilingi 23,552, 897.60 .  Pia Mabweni 2 ambayo yako katika hatua za kenchi yatagharimu kisi cha shilingi 150,000,000. 

Changamoto kubwa ni gharama ya vifaa bei zake kubadilika mara kwa mara, pia gharama za ujenzi zimeonekana kuwa juu kutokana na eneo lenyewe kuwa mlimani . Mkuu wa wilaya aliaomba wadau na wananchi wajitokeze kusaidia ujenzi na vifaa vya shule hiyo. “nia yetu ni kuifanya shule ya mfano ili iweze kushindana na shule kama Feza na St Francis na zinginezo zinazo fanya vizuri, la msingi ni kuboresha miundo mbinu” 
Mhe Kasesela pia alimshukuru sana Bwana Tibba Guyayi kutoka Dar Es salaam ambaye ameahidi kutoa kompyuta 2 kwa ajili ya shule na kuwaomba wengine waige mfano wa bwana Guyayi.
 Ujenzi wa madarasa na mabweni katika shule ya sekondari Tagamenda 
 Mkuu wa wilaya Iringa Mhe Richard Kasesela akiwa katika  ziara ya kukagua madarasa na mabweni katika shule ya sekondari Tagamenda
 Mkuu wa wilaya Iringa Mhe Richard Kasesela akitoammaagizo wakati wa ziara yake ya kukagua madarasa na mabweni katika shule ya sekondari Tagamenda

 Mkuu wa wilaya Iringa Mhe Richard Kasesela akiendelea  kukagua madarasa na mabweni katika shule ya sekondari Tagamenda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...