Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Nyabaganga Talaba amewataka Watanzania kupenda kununua bidhaa zinazozalishwa hapa nchini ili kwenda sambamba na sera ya Tanzania yenye viwanda pamoja na kuimarisha uchumi wetu.

Amesema hayo wakati akizindua Baraza la Biashara Wilaya ambapo alishangazwa na baadhi ya kuamini kuwa bidhaa zinazozalishwa nchini hazina ubora na hivyo kukimbilia za nje.

Talaba ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Biashara Wilaya alisema bidhaa zetu zina ubora kutokana na kutumia malighafi halisi akitolea mfano viatu vinavyozalishwa na Watanzania ukilinganisha na vinavyotoka nje ya nchi ambavyo vingi havidumu.

”Tufike mahali sasa tununue bidhaa zetu ili fedha izunguke kwani tutaimarisha uchumi na kama tunavyofahamu lengo la Rais katika sera ya nchi ya viwanda anataka tununue bidhaa zetu.

Mkuu huyo wa wilaya alilitaka baraza liwe chachu ya kusukuma sera ya nchi ya viwanda na kuibua fursa ambazo wananchi waananchi wanaweza kuzitumia na kuanzisha biashara.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba akizungumza wakati wa kikao cha kwanza cha Baraza la Biashara Wilaya alilozindua rasmi. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Shinyanga (SHIREMA), Gregory Kibuse). 
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba akiangalia bidhaa za vigae zilizotengezwa kwa kutumia majani ya mkonge wakati wa maonesho ya wajasiliamali kabla ya uzinduzi wa Baraza la Biashara Kishapu.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba akiangalia bidhaa za vigae zilizotengezwa kwa kutumia majani ya mkonge wakati wa maonesho ya wajasiliamali kabla ya uzinduzi wa Baraza la Biashara Kishapu. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...