MRADI wa Bomba la Mafuta Mkoani Tanga umefikia kwenye hatua ya wataalamu kukagua njia itakayopitisha miundombinu ya bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.

Hatua hiyo imekuja baada ya serikali ya Tanzania na Uganda kutiliana saini ya mkataba baina ya nchi na nchi (Iga) kukamilika.

Hayo yalisemwa leo na Mwanasheria Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini Tanzania (TPDC), Kelvin Gadi wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda lao ambalo lipo eneo la mwahako jijini Tanga kunakofanyika maonyesho ya tano ya biashara kimataifa.

Alisema tayari wameshafanya maamuzi yameshakamilika wataalamu wanafanya tathimi ya udongo katika njia ambayo bomba hilo litapita kwa taarifa ya awali njia iliyopatikana upana mita 200 na baadae watalaamu wataipunguza mpaka 100.

Awali akizungumza kuhusiana na mradi huo, Afisa Uhusiano wa Shirika hilo, Augustino Kasale alisema mradi huo utapita katika mikoa nane ya Tanzania na kuzalisha ajira 10000 za kudumu na muda mfupi.

Alizitaja fursa ambazo zitakuwa moja kwa moja ni hutoaji huduma wakati wa ujenzi, ajira za muda mfupi na moja kwa moja, fursa za usafirishaji ikiwemo kuufungua mkoa wa Tanga kiuchumi.

“Hivyo hivi sasa wananchi wa mkoa wa Tanga wanapaswa kujiandaa na ujio wa Bomba la Mafura ghafi kutoka hoima nchini Uganda hadi Mkoani Tanga “Alisema.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.


 Afisa Uhusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Augustino Kasale kulia akimueleza jambo  Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage kushoto wakati alipofungua maonyesho ya tano ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga.
 Mwanasheria Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini Tanzania (TPDC), Kelvin Gadi wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda lao ambalo lipo eneo la mwahako jijini Tanga kunakofanyika maonyesho ya tano ya biashara kimataifa.
 Afisa Uhusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Augustino Kasale akizungumza na waandishi wa habari leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...