Kituo cha East Africa Television (EATV) na East Africa Radio kwa udhamini wa Kinywaji cha Sprite, kiimeandaa mashindano ya mpira wa kikapu yanayojulikana kama ‘Bball Kings’.

Akizungumza na Waandishi wa habari mapema jana jijini Dar,Mwakilishi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania - Tanzania Basketball Federation (TBF),  Mwenze Kabinda alisema kuwa 
yanatarajia kufanyika katika viwanja tofauti ndani ya Jiji la Dar es Salaam kuanzia mwezi huu wa Mei na kufikia tamati mwezi Julai mwaka huu.

Kabinda alisema kuwa mashindano hayo yatashirikisha timu mbalimbali za mpira wa kikapu kutoka pande mbalimbali za Tanzania.

" Dhumuni kuu la mashindano haya ni kuutangaza na kuibua vipaji vipya katika mchezo wa kikapu hapa nchini.Mashindano haya yamepatiwa kibali kuendeshwa hapa nchini kwa kuzingatia sheria za Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania - Tanzania Basketball Federation (TBF),na kwamba mashindano haya yatakuwa na hatua kuu saba",alisema Mwenze Kabinda.
 Meneja Mauzo na Masoko (EATV),Ronald Mbowe  akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari mapema jana jijini Dar kuhusiana na zawadi mbalimbali zitakazotolewa katika Mashindano hayo,na pia vigezo vitakavyotumika katika ushiriki wake.
 Afisa Masoko wa Sprite-Tanzania,Pamela Lugenge. (kulia),ambao ndio wadhamini wa Mashindano hayo,akizungumza mbele ya Waandishi wa habari,mapema jana jijini Dar,naona ya kuyaboresha mashindano hayo ambayo yamekuwa yakiwavutia mashabiki wengi wa mchezo huo
Pichani kushoto ni Mwakilishi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania - Tanzania Basketball Federation (TBF),  Mwenze Kabinda akitoa ufafanuzi kuhusiana na mashindano ya mpira wa kikapu yanayojulikana kama ‘Bball Kings’.,mbele ya Waandishi wa habari mapema jana,ambapo mashindano hayo yanatarajiwa kuanza kurindima ndani ya mwezi huu wa Mei na kufikia  tamati mwezi Julai,mwaka huu.Pichani kati ni Meneja Mauzo na Masoko (EATV),Ronald Mbowe na kulia ni Afisa Masoko wa Sprite-Tanzania,Pamela Lugenge. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...