THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MUHIMBILI KUANZA UPANDIKIZAJI WA VIFAA VYA USIKIVU JUNI, MWAKA HUU

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imesema kwamba huduma ya kupandikiza vifaa vya usikivu kwa watoto wenye matatizo ya masikio na watu wengine itaanza kutolewa Juni, mwaka huu.Huduma ya upandikizaji huo utaipunguzia serikali gharama za kuwapeleka wagonjwa wenye matatizo hayo nchini India.

Kauli hiyo imetolewa leo na Daktari Bingwa wa Masikio, Pua na Koo katika Hospitali ya Muhimbili, Edwan Liyombo wakati wa kutoa elimu kwa wazazi wa watoto wenye matatizo ya masikio jinsi ya kutunza vifaa vya usikivu kwa watoto waliopatiwa huduma hiyo.

Dk Liyombo amesema kwamba huduma itaanza kutolewa nwezi Juni, mwaka huu na kwamba Hospitali ya Muhimbili imeboresha miundombinu na tayari imenunua vifaa kwa ajili ya kuanza kwa huduma hiyo.

Kuhusu gharama za mtoto mmoja kuwekewa kifaa cha usikivu amesema ni ndogo kuliko akiachwa bila kupatiwa huduma hiyo kwani maisha yake yote atakuwa hasikii wala hataweza kupata uelewa wa masomo shuleni.

“Sisi tunaona hakuna gharama ya mtoto kuwekewa kifaa cha usikivu kwa sababu huduma hii ataitumia katika maisha yake yote na akipelekwa shule atakuwa na uwezo wa kusikia na kuzungumza, kwa kifupi atakuwa sawa kama watoto wengine ambao hawana matatizo ya kusikia,” amesema Dk Liyombo.

Akizungumzia lengo la kuwaita wazazi wa watoto wenye matatizo ya kutokusikia, Dk Liyombo amesema ni kuwaelekeza jinsi ya kutunza vifaa hivyo na endapo vina matatizo wanapaswa kutoa taarifa ili virekebishwe.
Amewataka wazazi wenye watoto wenye matatizo ya kusikia kuwapeleka katika hospitali hiyo kwa ajili ya kupatiwa huduma na pia amewataka kinamama wajawazito kuudhuria kliniki ili kuchunguzwa afya zao pamoja na mtoto kwa lengo la kuzuia mtoto kuzaliwa na tatizo la usikivu.

 Daktari Bingwa wa Masikio, Pua na Koo, wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Edwin Liyombo akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu huduma ya upandikizaji wa vifaa vya usikivu kwa watoto wenye matatizo ya masikio. Kutoka kushoto ni Maneja wa Bidhaa, Shalini Srivatsan wa Kampuni ya Vanguard (T) Limited na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Nitesh Patel.
 Baadhi ya wazazi wenye watoto ambao wana matatizo ya usikivu wakimsikiliza Dk. Liyombo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Maneja wa Bidhaa, Shalini Srivatsan wa Kampuni ya Vanguard (T) Limited akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu namna wanavyosaidia jamii
 Watoto wenye matatizo ya usikivu wakiwa kwenye mkutano huo leo.
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa Hospitali ya Muhimbili, Aminiel Aligaesha (kulia), Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanguard (T) Limited, Nitesh Patel na Maneja wa Bidhaa wa kampuni hiyo, Shalini Srivatsan (kushoto) wakimsikiliza Dk Liyombo wa Muhimbili kabla ya kuanza kwa mkutano na waandishi wa habari wakiwamo wazazi wa watoto wenye matatizo ya usikivu. Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).