NA HAJI NASSOR, PEMBA

ABIRIA waliokuwa wakitokea Unguja, wafanyakazi wa serikali na taasisi binafsi pamoja na wananchi wengine, juzi walilazimika kusubiri kwa dakika 45, kwenye eneo la mpakani baina ya wilaya za Mkoani na Chakechake, kufuatia mti aina ya Muwembe kukatika na kuziba barabara.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, abiria na wananchi hao walisema, baada ya kuteremka meli bandari ya Mkoani, walipanda gari za abiria ili kuelekea kwenye mkaazi yao, ingawa walipofika mpakani walikwama.

Walisema walikaa hapo tokea majira ya saa 10:30 hadi saa 11:15 ndipo walipofanikiwa kupita baada ya taasisi kadhaa wakiwemo idara ya misitu kukakata Muwembe.Walisema kama sio taasisi za serikali zikiwemo KZU, Idara ya misitu na wananchi wanaoishi karibu na eneo hilo la Vuleni kushirikiana wengeutumia hadi saa 1:30.

Mmoja kati ya abiria aliekuwa akitokea Unguja, Juma Mshihiri Hassan mkaazi wa Konde, alisema baada ya kufika hapo walishuhudia foleni ya gari zaidi ya 30 na waliarifiwa kwamba barabara imefungika, kutokana na kuanguka Muwembe katikati.
Wananchi wa kisiwa cha Makoongwe wilaya ya Mkoani Pemba, wakiwa safarini ndani ya mashua yenye mashine, wakitokea Mkoani mjini kwenda kijijini kwao, ambapo hayo ndio maisha yao ya kila siku, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
Ipo haja kwa wazazi na walezi, kuwa makini na maeneo wanayocheza watoto wao, ambapo mtoto ambae hakupatikana jina lake, akikata tawi, alilolikalia karibu na skuli ya Makoongwe wilaya ya Mkoani
Mwandishi wa Shirika la Magazeti ya Serikali ofisi ya Pemba Haji Nassor, akizungumza na Mwenyekiti Jumuia ya Sanaa, Elimu ya Ukimwi na Mazingira JSEUMA, Juma Ali Mati juu ya hatua waliofikia, ndani ya jumuia yao, kuhusu kuwaelimisha wananchi kupanda miti na kuhifadhi mazingira.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...