THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MVUA ZAHARIBU MIUNDOMBINU YA BARABARA MKURANGA

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Kutokana na mvua zinazoendelea katika maeneo tofauti barabara mbili zimekata mawasiliano na kufanya baadhi huduma za kijamii kushindwa kufanyika.

Barabara zilizokata mawasiliano ni barabara ya Chamanzi kwenda Kibamba pamoja na barabara ya barabara ya Mkuranga kwenda Hoyoyo.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Dodoma, Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega amesema kuwa hali ya barabara katika jimbo lake ziko katika hali mbaya kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Amesema kuwa ameomba barabara ya Kimazichana kwenda Kibamba kuingizwa katika barabara za Tanroads ili ziweze kuangaliwa kutokana umuhimu wake katika uchumi wa nchi.

Diwani wa Kata ya Tengerea , Shaban Manda amesema kuwa barabara ya Mkuranga kwenda Hoyoyo makaravati yaliyowekwa hayawezi kuhimili mvua ikiwa kubwa.

Amesema wakandarasi wanatakiwa kushirikisha wananchi katika uwekaji wa madaraja na makaravati kutokana na wao ndio wanajua sehemu zenye matatizo.Manda amesema kuwa wakati mwingine sehemu zinazowekwa makaravati hayana umuhimu ndio maana mvua zikinyesha nayo yanakwenda na maji .

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kimazichana , Omary Ndeu amesema hali mbaya kwa wananchi wa Mbezi na Kibamba hawawezi kufika kimazichana ambapo huduma za kijamii na biashara ndio zinafanyika.
Wananchi wakishuka katika daladala inayofanya safari zake Kibamba , Kimazichana na Dar es Salaam kwa ajili ya kuvuka kutokana na barabara hiyo kukatika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Vijana wakitengeneza barabara ya dharula kwa ajili ya kupitisha magari na kupata kipato kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Picha zote na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
Barabara ya Mkuranga kwenda Hoyoyo ikiwa imekatika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Diwani wa Kata ya Tengerea, Shaban Manda akizungumza na Michuzi Blog juu ya barabara hiyo kukatika na kukatika kwa mawasiliano.