MWALIMU Commercial Bank PLC imezindua kampeni ya “Weka Akiba na Ushinde” kwa Wateja wake na wananchi kwa ujumla.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mei 18, 2017 wakati akizindua kampeni hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank PLC, Bw. Ronald Manongi alisema, “Draw hiyo ipo wazi kwa wateja wote waliopo na watakaojiunga na sifa kubwa ya kuingia kwenye draw hiyo ni kwa mteja aliyepo au anayejiunga, kuweka akiba ya Shilingi 50, 000 au zaidi.” Alisema Bw. Manongi.

Akifafanua zaidi Afisa huyo Mtendaji Mkuu wa benki hiyo alisema, kampeni hiyo ambayo itawawezesha wateja kupata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali kila mwezi kwa kipindi cha miezi miwili.“Mteja anapoweka akiba (fedha), kiasi cha Shilingi 50,000 au zaidi, atapata alama, (Point) moja itakayomuwezesha kushiriki kwenye draw.” Alisema.

Alisema, kadiri Mteja anapoweka akiba zaidi ndivyo Anavyojiwekea nafasi nzuri ya kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo IPADS na vocha za manunuzi zenye thamani ya Shilingi 100,000 na kwamba kila itakapochezeshwa draw hiyo, washindi wanane (4) na kujishindia zawadi mbalimbali.

Akielezea hudma za benki hiyo, Bw.Manongi alifafanua kuwa Mwalimu Commercial Bank inatoa gharama nafuu na rafiki za kibenki na ni suluhisho la kifedha kwa walimu, watumishi wa serikali na wananchi kwa ujumla na kutoa wito kwa Wateja wapya kuja kufungua Akaunti na kuweka akiba ili wapate nafasi ya kuingia kwenye draw hiyo.

Naye Mkuu wa kitengo cha Biashara na Masoko wa Benki hiyo, Bw. Valence Luteganya alisema, “Huduma za kibenki za MCB ni bora na nafuu, tunawahakikishia wateja wetu waje kufanya maamuzi ya kifedha yaliyo sahihi kwani tunatoa huduma mbalimbali za kibenki zilizo nafuu.” Alisema na kuongeza kuwa MCB pia inatoa huduma za ATM zilizounganishwa na mtandao wa Umoja switch ambao una ATM zaidi ya 200 nchi nzima.

“Lakini si hivyo tu pia huduma bora za kibenki kupitia simu za mkononi (Mobile Banking), huduma ya bure ya ujumbe wa SMS ukiwa na usalama na kuwawezesha wateja kupata taarifa za mara kwa mara kuhusiana na Akaunti zao. Hivyo natoa wito kwa wananchi kwa ujumla kuja na kujiunga na Benki yetu kwa huduma bora na za uhakika.” Alisema. 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank PLC, Bw. Ronald Manongi, (katikati), akiwa na Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko, Bw. Valence Luteganya, (kulia) na Meneja Masoko, Bi. Rahma Ngassa, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mei 18, 2017.
Mkuu wa kitengo cha Biashara na Masoko wa Benki hiyo, Bw. Valence Luteganya, akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari,mapema leo jijini Dar kuhusiana na kampeni yao wanayotarajia kuianza hivi karibuni.

Waandishi wa habari wakisikiliza maeleoza mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank PLC, Bw. Ronald Manongi kuhusiana na namna kampeni hivyo itakavyofanyika.

Meneja Masoko wa benki hiyo, Bi. Rahma Ngassa,(kushoto), akizungumzia ubora wa huduma za kibenki kwenye benki hiyo na namna wanavyoweza kutoa huduma ya ushauri mbalimbali kwa wateja wao,Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa MCB, Bw. Manongi.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...