THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Mzumbe, Norway Waendesha Utafiti Kuhusu Masuala ya Kodi

Profesa Honest Prosper Ngowi akiwaelekeza baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe kuhusu utafiti unaoangazia masuala ya kodi. Kulia ni Profesa Arne Wiig akitoa maelekezo kwa mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho. Utafiti huo unafanywa kwa ushirikiano kati ya Taasisi ya Christian Michelsen Institute (CMI) ya Norway na Chuo Kikuu Mzumbe cha nchini Tanzania.

Wanafunzi wa Mzumbe Dar Es Salaam wakifanya shughuli za utafiti kwa vitendo katika mradi wa utafiti wa mambo ya kodi. Mradi huu ni ushirikiano kati ya taasisi ya Christian Michelsen Institute (CMI) ya Norway na Chuo Kikuu Mzumbe. 

Unafadhiliwa na Baraza la Utafiti la serikali ya Norway na upo katika mwaka wa mwisho katika miaka yake mitatu. Professor Ngowi wa Mzumbe ni mtafiti mkuu katika mradi huu Tanzania. Watafiti kutoka Norway waliokuwepo Mzumbe ni Prof. Odd Fjeldstad na Prof. Arne Wiig. 

Katika utafiti huu wanafunzi walijibu maswali mbalimbali yahusuyo kodi. Matokeo yake yatatumika kushauri mamlaka kuhusu mambo kadhaa ya kodi Tanzania. Utafiti wa aina hii unafanyika pia Angola na Zambia.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe wakiendelea na utafiti huo jijini Dar es Salaam jana.
Wanafunzi wengine wakijadiliana jambo katika Chuo Kikuu cha Mzumbe ambako utafiti huo unaendelea leo.