THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe.William Ole Nasha azindua Wiki ya Unywaji maziwa Kitaifa

Ndugu Hussein Mapugilo mmoja wa wawakilishi wa GESAP DAIRY MILK, akitoa maelezo kwa Mh. Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mh. Ole Nasha, kuhusu shughuli zinazofanywa na Kiwanda hicho, wakiwa pia na malengo ya Uanzishwaji wa kiwanda cha Usindikaji Maziwa katika Wilaya ya Misenyi, hii ikiwa pia ni katika kuijenga Tanzania ya Viwanda.
Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe.William Ole Nasha akisaidiwa na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Kagera  akikata utepe kuashiria Kuanza kwa Wiki ya Unywaji maziwa Kitaifa. Maadhimisho haya yanafanyika katika viwanja vya Kyakairabwa, Manispaa ya Bukoba. 


Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe.William Ole Nasha akizungumza na mfugaji wa ng'ombe wa kisasa kutokea wilayani Misenyi Bi Haulath Athumani Mfugaji 

Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe.William Ole Nasha  akipata maelezo katika Banda la NARCO
 Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe.William Ole Nashaakipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wawakilishi Shirika la Maendeleo ya Wakulima (MAYAWA). 

Wasanii nyota wa Bongo Fleva wa Bukoba. Kushoto ni msanii Shemela akiwa na na Msanii Bk Sundaywakimwaga mistari
Kikundi cha ngoma za utamaduni cha Kakaku band kikitumbuza kwenye sherehe hizo za uzinduzi wa kunywa maziwa kitaifa.
Picha zote na Abdullatif Yunus wa Globu ya Jamii, Bukoba
Habari kamili BOFYA HAPA