Treni ya abiria iliyokuwa ikitokea jijini Dar es salaam kwenda Mikoa ya Tabora, Mwanza na Kigoma imepata ajali usiku wa kuamkia leo katika eneo la stesheni ya Mazimbu Mkoani Morogoro.

Kwa mujibu wa Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Reli Tanzani, Midladjy Maez amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa tano usiku baada ya Mabehewa matatu kuacha njia na mengine manne kuegama na kusababisha abiria mmoja aliyetambulika kwa jina la Ashura Mrisho aliyekuwa akitokea Ngerengere kwenda Tabora kujeruhiwa baada ya kuangukiwa na mizigo. 
Bw. Maez amesema mabehewa 13 yaliyokuwa katika treni hiyo tayari yamerejeshwa Morogoro kufanyiwa ukarabati na abiria wanafanyiwa utaratibu wa kuwapangia usafiri mbadala wa kuwafikisha wanakokwenda, ikiwa ni pamoja na kukodishiwa mabasi.
Amesema taarifa zaidi zitafuata wakati Uongozi wa TRL, Wahandisi na Mafundi wa reli wakishughulikia ajali hiyo. 
mabehewa ya treni ya  abiria iliyokuwa ikitokea jijini Dar es salaam kwenda Mikoa ya Tabora, Mwanza na Kigoma baada ya  ajali usiku wa kuamkia leo

 Sehemu ya abiria wa treni iliyokuwa ikitokea jijini Dar es salaam kwenda Mikoa ya Tabora, Mwanza na Kigoma imepata ajali usiku wa kuamkia leo.
Mabehewa  ya treni iliyokuwa ikitokea jijini Dar es salaam kwenda Mikoa ya Tabora, Mwanza na Kigoma baada ya  ajali usiku wa kuamkia leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...