KATIBU MKUU wa chama cha National  Reconstruction Alliance (NRA) Hassan Almas Kisabya (pichani kulia) ametoa pole kwa wafiwa,wakazi wa Arusha na Tanzania kwa ujumla kutokana na msiba mkubwa uliotokea Leo na kusababisha vifo vya wanafunzi   huko Karatu.
Akiongea na wanahabari ofisini kwake, Almas amesema,NRA wamepokea kwa mstuko taarifa hiyo ya ajali na vifo vya wanafunzi ambao ni nguvu kazi ijayo ya Taifa letu.
Kwa niaba  ya NRA, Almas amewataka wazazi ,Ndugu ,jamaa ,wana Arusha na watanzania kuwa na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.
Pmoja na salama hizo za pole, Almas amewataka madereva kuwa makini wanapokuwa barabarani ili kupunguza ajali zinazochangia vifo vingi vinavyopoteza hazina ya Taifa.
"Vijana hawa ndio hazina ya taifa hili, na ndio akiba ya ujuzi na utaalamu wa taifa,ajali hii imepoteza wabunge,mawaziri, walimu, madaktari ,wachumi,wanasiasa,askari ,marubani na hata wanasayansi wa miaka ijayo,huu ni msiba mkubwa kwa Taifa letu",amesema Almas.
Katibu Mkuu huyo ameliomba jeshi la polisi kuendelea kutoa elimu ya usalama barabarani ili kupunguza ajali na  amewashauri wanahabari kuandaa makala maalum katika vyombo vyao vya habari juu ya suala zima la usalama sio  makala za siasa pekee.
Alisema"nyie wana Habari ni wadau wakubwa sana wa usalama barabarani maana nanyi  ama jamaa zenu ni wasafiri, madereva,mnapotumia muda mwingi kuandika makala za siasa pia muandike Makala za usalama barabarani  ili kulisaidia jeshi la polisi ktk kazi hii ya kutoa elimu"
Almas pia amemtaka mkuu wa kitengo cha usalama Barabarani kukutana na wanasiasa ili kubadilishana mawazo juu ya kushirikiana nao katika kutoa elimu hiyo kwa wanachama wetu katika mikutano yao ya kisiasa inayohudhuriwa na watanzania wengi.
"Natoa ushauri kwa Kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani Kamanda Mohamed Mpinga kukutana na viongozi wa juu wa vyama vya siasa ili kubadilishana uzoefu,kutoa mafunzo mafupi na kutupatia vipeperushi vya elimu ya usalama barabarani ili tuwapatie wanachama wetu katika mikutano yetu ya kisiasa" ,alisema Almas.
Alijikita zaidi na kutoa mfano wakati wa uongozi wa IGP mstaafu Said Mwema,  suala la utii wa sheria bila shuruti wanasiasa walikuwa wakikutana na kubadilishana uzoefu juu ya masuala ya usalama na hatimaye kuwapatia vipeperushi vya elimu hiyo utii wa sheria nao waliweza kuwapa elimu hiyo wanachama wao., hili sio jambo la jeshi pekee maana jeshi lina kazi nyingi na muhimu ,nao kama wanasiasa wanao wajibu wa  kusaidia jeshi letu.
KATIBU MKUU wa chama cha National  Reconstruction Alliance (NRA) Hassan Kisabya Almas akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani na kuwapa pole watanzania kwa msiba uliotokea jana wa vifo vya wanafunzi vilivyotokea Mkoani Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...