*Asema utu, maendeleo na maisha bora havipatikani kwa fedha

MAKAMU MKUU wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Rwekaza Mukandala amewataka vijana wanaohitimu kidato cha sita nchini wawe makini na wasikubali kusombwa na mawimbi ya dunia.

Ametoa wito huo jana (Jumamosi, Mei 14, 2017) wakati akizungumza na wahitimu 237 wa kidato cha sita wa shule ya sekondari ya St. Joseph Cathedral kwenye mahafali ya sita ya shule hiyo yaliyofanyika shuleni hapo, jijini Dar es Salaam.

Prof. Mukandala alisema: “Kwa hatua mliyofikia kila mmoja anapaswa atafakari kwa kina wito wake kimaisha. Kuweni makini, msisukumwe na mawimbi ya dunia na kujikuta mmepoteza ndoto zenu,” alisisitiza.

“Kuhitimu kidato cha sita si jambo dogo. Ni hatua ya kuwaongiza kujiandaa na utu uzima ikiwemo kujiunga na elimu ya vyuo vya juu na kuingia kwenye ndoa. Ni muda wa kutathmini yale uliyopitia na kutafakari maisha yako ya baadaye. Ni fursa ya kutoa shukrani kwa Mungu, kwa wazazi na walimu ambao walifanya kazi kwa umakini na kujitoa ili mfikie hatua nzuri mliyopo sasa,” alisema.

Alisema kuanzia sasa kila mmoja wao anapaswa kujiamini, kujituma zaidi na kujiona kuwa ana wajibu wa kujiletea maendeleo binafsi. “Mnapaswa kuepuka mwenendo wa kujiona mnyonge, au mtu asiyeweza kutimiza ndoto zake. Jenga tabia ya kuwa makini na maisha yako, jali mazingira yako na maendeleo yako,” alisisitiza.

Aliwataka wahakikishe wanakuchukua hatua mahsusi na kupata taarifa sahihi kuhusu taaluma wanazozitaka. Aliwataka wawe waadilifu na wenye heshima kwa watu wote lakini pia akawaasa juu ya maisha ya kutaka kupata fedha kwa haraka na kujilimbikizia mali.

“Epukeni rushwa na ufisadi. Mnatakiwa kujua kuwa utu, maendeleo na maisha bora havipatikani kwa fedha ingawa nayo ni muhimu katika maisha. Msitegemee kuishi kwa kuzingatia mambo makubwa yanayopimika kwa fedha,” alisema.
Mkuu wa Shule ya St. Joseph Cathedral, Sista Theodora Faustine akimkabidhi zawadi na cheti, Prof. Rwekaza Mukandala ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya sita ya kidato cha sita, ili ampatie mhitimu. Mahafali hayo yalifanyika Jumamosi, Mei 13, 2017 shuleni hapo. (Picha na Irene Bwire)
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Prof. Rwekaza Mukandala ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya sita ya kidato cha sita ya Shule ya St. Joseph Cathedral, akizungumza na wahitimu (hawapo pichani). Mahafali hayo yalifanyika Jumamosi, Mei 13, 2017 shuleni hapo. (Picha na Irene Bwire).  
Viranja wa darasa la PCM, Martin na Nsobya Musona wakipokea zawadi ya keki kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Prof. Rwekaza Mukandala ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya sita ya kidato cha sita ya Shule ya St. Joseph Cathedral, yaliyofanyika Jumamosi, Mei 13,2017) shuleni hapo. 
Baadhi ya wazazi, walezi na ndugu walioshiriki mahafali ya sita ya kidato cha sita ya shule ya sekondari ya St. Joseph Cathedral yaliyofanyika Jumamosi, Mei 13, 2017 shuleni hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...