Mratibu wa Masuala ya
Usalama wa Afya, Mazingira na Udhibiti
wa Ubora kutoka Kampuni ya Puma Energy, Rehema Madoffe akimvisha Abubakar
Selemani mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Ungindoni iliyopo
Kigamboni Dar es Salaam moja ya fulana inayoakisi mwanga ikiwa ni sehemu ya
shehena iliyotolewa kwa shule hiyo kwa
ushirikiano na Taasisi ya Amend Tanzania kusaidia kampeni ya kupunguza
ajali za barabarani hususani kutetea maisha ya watoto wa shule jana ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya
Usalama barabarani ya Umoja wa Mataifa(UN-Global Road Safety Week)
Ofisa Mipango wa Taaasi ya Amend Tanzania, Neema Swai
akigawia fulana maalum zinazoakisi mwanga kwa waendesha bodaboda wa Manispaa ya
Kigamboni mkoani Dar es Salaam, jana, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya
Usalama barabarani ya Umoja wa Mataifa(UN-Global Road Safety Week)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...