Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Raia wa Kenya, Samson Mbaria Pirias maarufu kama Babaa, 38, na raia wa Tanzania, Lohelo Boniphace Mwabulanga anayejulikana zaidi kama Diblo, 43, wamepandishwa kizimbani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,  wakikabiliwa na tuhuma za kusafirisha binadamu kutoka nchini Kenya kwenda Afrika Kusini kuwafanyisha kazi kwa lazima.

Mwendesha Mashtaka Wakili wa Serikali, Elia Athanas amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 4(1) (a) na (1) (2) (c) na 4 cha sheria ya kusafisha binadamu sura ya sita ya mwaka 2008.

Wakili Athanas amedai kuwa, Februari 28,mwaka huu, huko Chanika wilaya ya Ilala washtakiwa hao walikutwa wakiwasafirisha watu 11 kutoka Kenya kwenda Afrika Kusini kwa lengo la kuwafanyisha kazi kinguvu.

Aliwataja watu hao kuwa ni Dhaha Maliya All, Hassen Gales Omar, Ahmed Lobiso Abdi,Dhawil Ayantu Duri, Omar Yahye Mohammed, Hikma Ibrahim Omar, Istahil Ali Shukri, Rashid Omar Yusuf,Abdul Khalid Asiis, Abbdulah Sartu na Hassen Guled Omar.

Hata hivyo, washtakiwa hao wote wawili wamekana tuhuma hizo na wamerudishwa rumande kwa sababu shtaka linalowakabili la kusafirisha binadamu ni moja kati ya mashtaka yasiyo na dhamana.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa shauri hilo bado haujamalika. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 17,mwaka huu kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya kutajwa tena.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...