Na Mwamvua Mwinyi,Pwani 

MKUU wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo,amemaliza ziara yake ya kutembelea wilaya sita kimkoa,ambapo amehimiza mambo makuu manne ikiwemo ulinzi na usalama,uwekezaji,kilimo cha matunda na korosho.

Aidha amekemea migogoro ya wakulima na wafugaji ambayo imekuwa ikigharimu maisha ya watu na wengine kujeruhiwa pasipo sababu za msingi.

Akimaliza ziara yake wilayani Kibaha,mhandisi Ndikilo,alieleza mkoa wa Pwani una viwanda vitatu vikubwa vya kusindika matunda kwa sasa ambavyo endapo wakulima watavitumia watanufaika kwa kiasi kikubwa.

Alisema,kiwanda cha Bakhresa ambacho kipo Mwandege -Mkuranga kimeshaanza kazi na kile cha Elven Agri co.ltd kilichopo kata ya Mapinga -Bagamoyo huku cha Sayona kinachojengwa kata ya Mboga kikiwa kwenye hatua za mwisho za ujenzi.

Mkuu huyo wa mkoa alisema kiwanda cha kusindika matunda cha Bakhresa kina uwezo wa kusindika tani 350 za matunda kwa siku na uwekezaji wake umegharimu sh.bil.261.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo, akiwa ametembelea shamba la mfano la zao la biashara la korosho lililopo Ruvu JKT, wilayani Kibaha. (picha na Mwamvua Mwinyi) . 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...