Aliyekuwa  kuwa Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, Steven  Wassira  akiwa katika jengo la Mahakama ya Rufaa jijiji Dares Salaam akizungumza jambo na baadhi ya mawakili kabla ya kusikiliza kwa Rufaa ya kesi yake dhidi ya Mbunge wa Bunda mjini Ester Bulaya.  Katika kesi hiyo jopo la majaji watatu  wa Mahakama ya Rufaa limepanga kuendelea na kesi hiyo Jumatatu ijayo ya Aprili 15, mwaka huu. Uamuzi huo umetolewa  leo  Aprili 11, mwaka huu katika Mahakama hiyo  baada ya  Pande zote mbili  kutoa maelezo  ya sababu za rufaa.
Wakili wa Mbunge  wa Jimbo la Bunda Mjini, Tundu Lissu  akizungumza  jambo na mara baada kikao kilichokuwa kinasikiliza ombi la rufaa lilifunguliwa na  wapigakura wanne wa Jimbo la Bunda, kupinga  hukumu ya  Mahakama Kuu Kanda ya  Mwanza, kuhusu ushindi wa mbunge wa jimbo hilo, Ester Bulaya.

Wakili  Constantine  Mutalemwa  akifafanua  jambo kwa baadhi  ya waandishi  wa habari  mara baada kikao kilichokuwa kinasikiliza ombi la rufaa lilifunguliwa na  wapigakura wanne wa Jimbo la Bunda, kupinga  hukumu ya  Mahakama Kuu Kanda ya  Mwanza, kuhusu ushindi wa mbunge wa jimbo hilo, Ester Bulaya.(PICHA NA MAGRETH  KINABO)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. MZEE WANGU USHAURI WANGU KWAKO NI NENO HILI;
    KUKUBALI KUWA UMESHINDWA NI SAHINI NYINGINE YA HESHIMA,
    DR JAMESSY

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...