Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL), imeanzisha safari zake kutoka Tabora kwenda mikoa ya Dodoma na Dar es Salaam kwa lengo la kurahisisha huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo katika mikoa hiyo na mikoa jirani. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa safari za ndege za kampuni hiyo mkoani Tabora, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, amesema kuwa kuanzishwa kwa safari hizo katika mikoa hiyo kutatanua wigo wa kibiashara na kukuza uchumi kupitia sekta mbalimbali ikiwemo za utalii na kilimo.

“Naamini wananchi wa mkoa wa Tabora na mikoa ya jirani, sasa mtanufaika kwa ujio wa ndege hii, matumaini yangu kwamba mtatumia usafiri huu ambao hautumii muda mrefu katika kurahisisha shughuli zenu za kibiashara na kijamii”, amesema Eng. Ngonyani.

Aidha, Naibu Waziri Ngonyani amewataka wananchi wa mkoa wa Tabora kutumia fursa ya ujio wa ndege hiyo kama chachu ya kuleta maendeleo katika mkoa huo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri, wakikata keki kama ishara ya kuzindua rasmi safari za Ndege za Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL), mkoani humo. 
Baadhi ya viongozi na wabunge wakiingia kwenye ndege aina ya Bombardier Dash 8 Q400 ya Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL), iliyotua kwa mara ya kwanza mkoani Tabora katika uzinduzi wa safari za ndege mkoani humo. 

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho, wakiwa ndani ya ndege kuelekea katika uzinduzi wa safari za ndege za Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL), mkoani Tabora. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...