Na Asteria Muhozya, Arusha
Wadau wa Madini nchini wametakiwa kujikita katika shughuli za ukataji na usanifu wa madini badala ya kusanifiwa nje ya nchi ili kuwezesha adhma ya Serikali ya Tanzania ya Viwanda kupitia Sekta ya Madini.
Hayo yalisemwa na Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamini Mchwampaka wakati wa kufunga Maonesho ya 6 ya Kimataifa ya Madini ya Vito yaliyofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 3-5 Mei,2017.
Aliongeza kuwa, uwepo wa shughuli za ukataji na unga'rishaji wa madini hayo nchini kutawezesha kuyaongezea thamani ikiwemo kupanua wigo wa ajira kupitia sekta ya madini.
" Tanzania ya sasa ni ya Viwanda. Na sisi sekta ya madini tuwe na viwanda vyetu vya kusanifu madini yetu hapa hapa nchini. Kwanza tutayaongezea thamani madini yetu lakini pia tutazalisha ajira kwa wingi," alisema Mchampaka.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (katikati), Waziri wa Madini na Maendeleo ya
Viwanda wa Nigeria Abubakar Bwari (wa
pili kulia), Katibu Mkuu wa Wizara ya
Madini na Maendeleo ya Viwanda wa Nigeria,
Abbas Mohamed (wa kwanza kulia) , Mwenyekiti wa Kamati ya Maonesho ya
Arusha Peter Pereira ( wa kwanza kushoto ) na Mwenyekiti wa Chama Cha
Wafanyabiashara wa Madini Tanzania Sam Mollel (wa pili kushoto) wakifuatilia
kutangazwa kwa washindi wa Mnada wa Madini ya Tanzanite.
Kamishna
wa Madini Tanzania Mhandisi Benjamin Mchwampaka (katikati) akikata kamba maalum
katika masunduku yaliyowekwa bahasha za walioomba kununua madini ya
Tanzanite kupitia mnada. Kulia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika la Madini la
Taifa, (STAMICO) Mhandisi Hamis Komba na kushoto ni Mwakilishi kutoka Kampuni
ya TanzaniteOne, Husein Gonga.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (kulia) akiangalia zawadi kabla ya kumkabidhi
Waziri wa Madini na Maendeleo ya Viwanda wa Nigeria, Mhe. Abubakar Bwari (kushoto).
Baadhi
wa washiriki wa Maonesho ya 6 ya Madini
ya Vito Arusha wakiwemo wanunuzi na wauzaji wakifuatilia hatua za kumpata
mshindi wa Mnada wa Madini ya Tanzanite.
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya SDK Limited, Bi. Susie Kennedy akimwonesha Waziri wa Madini na
Maendeleo ya Viwanda wa Nigeria, Mhe. Abubakar Bwari bidhaa za madini
zinazotengenezwa na kampuni hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...