Serikali
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
imeahidi kuajiri watumishi wa idara ya afya ili kujaza nafasi
zilizoachwa wazi na watumishi ambao wameondolewa katika utumishi wa umma
kwa kukosa sifa ya kuwa na vyeti halisi baada ya zoezi la uhakiki wa
vyeti nchini.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
ameyasema hayo jana wakati wa maadhimsho ya Siku ya Wauguzi Duniani
ambapo kitaifa imefanyika katika hospitali ya St. Gasper, Itigi Wilaya
ya Manyoni Mkoani Singida.
Waziri
Ummy amesema serikali inatambua mzigo mkubwa wa majukumu kutokana na
uhaba wa wauguzi ambao umesababishwa na baadhi yao kuondolewa katika
utumishi kwa kukosa vyeti halisi na hivyo imetenga bajeti ya kuajiri
wauguzi wa kutosha nchini huku akiahidi kutoa kipaumbele kwa mkoa wa
Singida.
“Kuna
baadhi ya Zahanati na vituo vya afya vimefungwa kwa kutokana na sakata
la vyeti feki, lakini pia tunatambua kuwa wauguzi hamtoshi na hivyo
kupelekea muuguzi mmoja kutoa huduma kwa wagonjwa wengi, hali hii
inapunguza ufanisi wenu na kuwanyima haki ya kupumzika”, ameongeza
Waziri Ummy.
Aidha
ameagiza waajiri wa utumishi wa umma na hasa halmashauri zote nchini
kupeleka maombi ya watumishi wa kada za afya ili wizara iweze kutangaza
nafasi hizo zijazwe na watanzania wenye sifa huku akisisitiza kuwa nia
ya serikali ya awamu ya tano ni kuboresha huduma za afya kwa wananchi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisisitiza jambo katika maadhimisho ya siku ya wauguzi iliyofanyika kitaifa katika hospitali ya St. Gasper Itigi, Mkoani Singida.
Wauguzi kutoka mikoa mbalimbali nchini wakila kiapo cha uuguzi katika maadhimisho ya siku ya wauguzi iliyofanyika kitaifa katika hospitali ya St. Gasper Itigi, Mkoani Singida.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiwakaribisha wauguzi kutoka mikoa mbalimbali nchini pamoja na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu katika maadhimisho ya siku ya wauguzi iliyofanyika kitaifa katika hospitali ya St. Gasper Itigi, Mkoani Singida.
Wauguzi kutoka mikoa mbalimbali nchini wakiandamana na kuonyesha ujumbe mbalimbali mbele ya Mgeni rasmi Waziri wa Afya Ummy Mwakimu katika maadhimisho ya siku ya wauguzi iliyofanyika kitaifa katika hospitali ya St. Gasper Itigi, Mkoani Singida.
Waziri wa Afya Ummy Mwakimu akisaini zawadi ya mafuta ya alizeti aliyopewa na wenyeji wake halmashauri ya Itigi katika maadhimisho ya siku ya wauguzi iliyofanyika kitaifa katika hospitali ya St. Gasper Itigi, Mkoani Singida.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...