Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.

Serikali kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji imesema kuwa Serikali ya India imeahidi kutoa dola milioni 500 kwa ajili utekelezaji wa miradi ya maji katika miji 16 ya Tanzania Bara na Zanzibar katika awamu ya tatu katika mwaka wa fedha 2017/18.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Eng.Isack Kamwelwe akijibu Swali la Mbunge wa Tumbatu Mhe.Juma Othman Hija leo Bungeni Mjini Dodoma.

“Katika bajeti ya mwaka 2016/17 Wizara yangu ilitoa taarifa ya mchango mkubwa inaoupata kutoka Serikali ya India ili kuboresha huduma ya Maji nchini kupitia mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali hiyoa”,Aliongeza Mhe.Kamwelwe.

Aidha katika awamu ya tatu hatua inayoendelea kwa sasa ni kufanya manunuzi ya Mhandisi Mshauri atayefanya mapitio ya usanifu wa miradi na uandaaji wa makabrasha ya zabuni kwa ajili ya ujenzi ambapo kazi ya ujenzi zinatarajiwa kuanza katika mwaka wa fedha 2017/18.

Amesema kuwa katika awamu ya kwanza Serikali ilipata dola za kimarekani Milioni 178.125 ambapo kazi zilizotekelezwa katika awamu hiyo ni upanuzi wa mradi mkubwa wa Ruvu Juu,Ujenzi wa bomba kuu kutoka Mlandizi hadi Kimara,Pia Ujenzi wa mfumo wa usambazaji maji katika Jiji la Dar es Salaam pamoja na ujenzi wa mradi Chalinze.

Katika awamu ya Pili Serikali ya India itatoa dola milioni 268.35 kwa ajili ya mradi mkubwa wa kutoa maji katika mradi wa KASHWASA kutoka kijiji cha Solwa kwenda katika miji ya Tabora,Igunga,Nzega,Tinde na Uyui pamoja na Vijiji 89 vinavyopitiwa na bomba kuu umbali wa kilomita 12 kila upande uku wakandarasi wa kutekeleza mradi huo wamepatikana na wapo katika hatua za utekelezaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...