THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetoa mkono wa pole kwa vifo vya wanafunzi, walimu na dereva Arusha

Na Othman Khamis Ame, OMPR
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetoa mkono  wa pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Mrisho Gambo kutokana na vifo vya Wafanuzi 32, Walimu pamoja na Dereva  wa Skuli ya Mchepuo wa Kingereza ya Luck Vicent kufuatia  Basi walilokuwa wakisafiria kupinduka katika Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.
Salamu hizo za pole zimetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein na Wananchi wote wa Zanzibar kufuatia msiba huo mzito kwa Taifa.

Balozi Seif Ali Iddi alisema Wananchi wa Zanzibar wamepokea kwa huzuni, masikitiko na mshtuko mkubwa taarifa ya ajali hiyo iliyotokea katika Kijiji cha Rhotia, Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha na kusababisha  vifo hivyo pamoja na Majeruhi kadhaa.
Alisema huo ni msiba mkubwa siyo tu kwa Wazazi, Ndugu na Jamaa wa Watoto hao bali pia ni kwa Taifa zima, kwani Watoto hao walikuwa nguvu kazi kubwa iliyotumainiwa kuja kulitumikia Taifa laWatanzania baada ya kumaliza Masomo yao.
Balozi Seif  alimuomba Mwenyezi Mungu awape wazazi na familia za Watoto hao moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hichi kigumu cha msiba na Wananchi wote Nchini Tanzania wako pamoja katika msiba huo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar pia alimuomba Mwenyezi Muungu mola wa viumbe wote azilaze roho za marehemu wote mahali pema pepono amin na wale majeruhi awaponyeshe haraka ili warudi kuendelea na maisha yao ya kila siku.