Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imelaani vikali kitendo cha mtoto wa miaka mitatu (jina limehifadhiwa), mkazi wa kata ya Rudete mkoani Geita, aliyeelezwa kwamba amejeruhiwa na mama wa kambo kwa kuchomwa moto mwilini akituhumiwa kuiba chakula alichobakiziwa baba yake.

Wizara imesikitishwa na tukio hili maana linakinzana na kaulimbiu ya Madhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Familia kwa mwaka 2017, ambayo pamoja na mambo mengine,  inasisitiza wazazi na walezi, kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao wa kuimarisha malezi kwa ajili ya ustawi wa watoto katika familia na jamii kwa ujmla.

Katika kutekeleza utoaji wa haki za Mtoto na ustawi wake, wadau wote wanaotoa huduma kwa mtoto wanasisitizwa kusimamia upatikanaji wa haki zote za msingi katika familia na jamii, ikiwemo haki ya kuishi, kulindwa, kuendelezwa, kushirikishwa na kutobaguliwa. 

Wizara inawaomba wananchi kote nchini kutoa ushirikiano katika kuwafichua wanaotenda vitendo vya unyanyasaji dhidi ya watoto kwa kutoa taarifa kwenye mamlaka husika, ili kuhakikisha wahusika wa vitendo vya ukatili wanachukuliwa hatua.

Napenda kutoa maelekezo kwa Maafisa Maendeleo, Ustawi wa Jamii wa kuhakikisha kuwa mtoto huyo anapatiwa huduma ya matibabu haraka ili kumrejesha katika afya njema. 

Kwa vile, jukumu la ulinzi na usalama wa mtoto linatekelezwa kwa ushirikiano mkubwa wa Polisi, tunaamini kuwa suala hili litafuatiliwa kuhakikisha kuwa watuhumiwa wa vitendo hivi vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya huyo mtoto mdogo wanapatikana.  

Azma ya Wizara yenye dhamana ya Watoto, ni kuhakikisha kuwa familia zinaendelea kuwa kitovu cha upatikanji wa haki, ustawi na maendeleo kwa maslahi ya watoto wetu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...