EFM redio kwa mara nyingine imehitimisha shindano la shika ndinga leo siku ya Jumamosi ya tarehe 6/5/2017 katika viwanja vya Tanganyika Packers - Kawe Jijini Dar es salaam ambapo washindi wawili wameondoka na magari aina ya Suzuki Carry maarufu kama Kirikuu ikiwa mmoja ni wa kiume na mwingine wa kike. 
Shindano hili lilianza tarehe 25/03/2017 ambapo lilifanyika katika wilaya 6 ambazo ni Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala, Bagamoyo na kibaha ambapo washindi wawili kutoka katika kila wilaya walizawadiwa Pikipiki kila mmoja aina ya Sanmoto. 
Efm redio kupitia shindano hili kwa ujumla limetoa pikipiki 12 pamoja na magari mawili ambayo hutumika katika shughuli za kiuchumi ikiwa kama njia ya kuwawezesha washindi kujiongezea kipato chao na kufanya maisha yao kukua kiuchumi.
 Burudani kutoka kwa Man Fongo, Sholo Mwamba, Madada 6, Virus, Yuda Msaliti na Chemical.
 Umati wa watu wakishuhudia shindano zima na burudani iliyoandaliwa na kituo cha E fm radio.

 Micheal Peter mshindi wa gari kwa upande wa wanaume akikabidhiwa mkataba na funguo wa gari lake na Bw Suleima Malele mkurugenzi wa uchumi na utawala alie mwakilisha Bi. Being’I Isaa Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC)

Joyce Daniel mshindi wa Gari aina ya Suzuki Caryy aka Kirikuu kwa upande wa wanawake.
Washindi kutoka wilaya ya Kigamboni, Temeke, Kinondoni, Ilala ,Kibaha na Bagamoyo wakiwa kwenye Pikipiki 12 aina ya San moto ambazo walikabidhiwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...